Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINE-Usalama

Israeli : watuhumiwa katika kifo cha kijana wa kipalestina wakamatwa

Polisi nchini Israeli imewatia nguvuni watu sita wanaohusishwa na mauaji ya kijana mmoja wa kipalestina alieuawa juma lililopita pale walipotaka kulipiza kisase dhidi ya wayahudi watatu waliouawa katika ukanda wa Gaza.

Polisi nchini Israeli imewatia nguvuni watu sita wanaohusishwa na mauaji ya kijana mmoja wa kipalestina alieuawa juma lililopita.
Polisi nchini Israeli imewatia nguvuni watu sita wanaohusishwa na mauaji ya kijana mmoja wa kipalestina alieuawa juma lililopita. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa hao wamefikishwa jana mbele ya jaji wa mahakama ya mji wa Petah Tikva kwa ajili ya kusomewa mashtaka. Duru za polisi zimesema kwamba watu hao wote ni vijana kutoka katika miji ya Jerusalam, Beit Shemesh, Adam na Scijordania karibu na jerusalem.

Wanamgambo wa kundi la Hamas.
Wanamgambo wa kundi la Hamas. REUTERS/Mohammed Salem

Maelfu ya wafuasi wa kundi la Hamas wameandamana jana katika ukanda wa Gaza wakipinga mauaji ya Mohammed Abu Khdeir alietekwa nyara na kuuawa kwa kuchomwa moto akiwa bado hai.

Akizungumza hapo jana, waziri mkuu wa Israrli Benjamin Netanyahu ameahidi kufuatilia wahusika wa tukio hilo ka kusikitisha na kuwafikisha kizimbani.

Watu hao wamekamatwa wakati huu ndege za kijeshi za Israeli zikishambulia vituo kadhaa katika ukanda wa Gaza na kuwauawa wapiganaji tisa wa kipalestina, wakati wakijibu mashambulizi ya roketi zinazo rushwa kutoka katika ukanda huo.

Kulingana na duru za kituo cha televisheni cha Chanel 10 cha nchini Israeli, watu hao sita waliokamatwa hapo jana, walishiriki katika maamdano ya kibaguzi muda mfupi kabla ya kutokea mauaji ambapo waandamanaji walidai kuuawa kwa waarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.