Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Siasa-Usalama

Israeli : mgawanyiko wajitokeza kufuatia mashambulizi dhidi ya Hamas

Ndege za kijeshi za Israeli zimeendesha mashambulizi ya anga zaidi ya thelathini katika ukanda wa Gaza usiku wa jumatatu kuamkia jumanne wiki hii. Mashambulizi hayo yameendeshwa kwa lengo la kukomesha kitendo cha kundi la Hamas cha kurusha makombora katika aridhi ya Israeli.

Mwoshi ukionekana katika katika mji wa  Rafah, kusini mwa ukanda wa Gaza, Julai 7 mwaka 2014.
Mwoshi ukionekana katika katika mji wa Rafah, kusini mwa ukanda wa Gaza, Julai 7 mwaka 2014. REUTERS/Abed Rahim Khatib
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Israeli wakipiga doria  jumatatu wiki hii, Julai 7, katika ukanda wa Gaza.
Wanajeshi wa Israeli wakipiga doria jumatatu wiki hii, Julai 7, katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Baz Ratner

Jeshi la Israeli limewatolea wito waisraeli waishio katika umbali wakilomita mraba 40 katika aridhi ya Palestina, kutoondoaka ndani ya nyumba zao, huku likiamuru kufungwa kwa kambi ya wanafuzi ambao wako likizo katika eneo kunakoendeshwa mashambulizi hayo.

Jeshi la israeli likendelea kumimina mabomu katika ukanda wa Gaza.
Jeshi la israeli likendelea kumimina mabomu katika ukanda wa Gaza. ( Photo : Jerry Lampen/ Reuters )

Kwa mujibu wa viongozi wa Palestina, zaidi ya maeneo 30 yalishambuliwa kwa muda wa saa moja, jumanne hii mapema asubuhi. Wizara ya afya imearifu kuwa watu tisa wamejeruhiwa kwa mabomu karibu na nyumba zilioko katika kijiji cha Khan Younis.

Watu waliyahama makaazi yao kabla kabla ya mashambulizi hayo. Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani, familia ziishio eneo hilo zilipewa taarifa mapema na afisa wa ujasusi wa jeshi la Israeli ya kufanyika kwa mashambulizi hayo.

Mashambulizi ya anga ya Jjeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza.
Mashambulizi ya anga ya Jjeshi la Israeli katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Mohammed Salem

Mgawanyiko umeanza kujitokeza katika serikali kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina. Waziri wa mambo ya nje wa Israeli, Avigdor Lieberman na waziri mkuu Benjamin Netanyahu hawaelewani kufuatia mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.