Pata taarifa kuu
UN-PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Palestina: Gaza: UN yalani mashambulizi ya Israeli

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani makombora yaliyorushwa kwenye shule moja ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili na kusababisha mauaji ya raia wa kipalestina wapatao kumi katika shambulio lililotekelezwa na askari wa Israeli.  

Msafara wa magari ya kijeshi ya Israeli yakijielekeza katika ukanda wa Gaza,  Ogasti 3 mwaka 2014..
Msafara wa magari ya kijeshi ya Israeli yakijielekeza katika ukanda wa Gaza, Ogasti 3 mwaka 2014.. REUTERS/Nir Elias
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limedhihirisha wazi ukiukwaji mwingine wa sheria za kimataifa ambapo pande zote mbili zililazimika kulinda usalama wa raia hao wa Palestina, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na majengo ya Umoja huo, amesema msemaji wa Katibu Mkuu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Wanajeshi wa Israeli wakikagua silaha zao kwenye mpaka wa Israeli na Gaza.
Wanajeshi wa Israeli wakikagua silaha zao kwenye mpaka wa Israeli na Gaza. AFP PHOTO / JACK GUEZ

Aidha, msemaji huyo amesisitiza kuwa lazima makaazi ya Umoja wa Mataifa yawe sehemu rasmi ya kukimbilia na si eneo la mapambano kama ilivyojitokeza mara kadhaa na kubaini kuwa lazima wahusika wa mashambulio hayo wachunguzwe na kuwajibishwa.

Katibu Mkuu Ban Ki Moon ameelezea kusononeshwa na ukiukwaji huo wa sheria za kimataifa na kubainisha kuwa serikali ya Israeli, licha ya kuwa imefahamishwa maeneo ambapo Umoja wa Mataifa umepiga kambi, askari wake wanaendelea kutekeleza vitendo vya uhalifu ambavyo rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa havikubaliki.

Tangu uvunjwaji wa makubaliano ya kusitisha mashambulizi ya tarehe mosi Agosti, mamia ya raia wa Palestina wameuwawa kutokana na mashambulizi hayo huku hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya zaidi katika ukanda wa Gaza, wakati ambapo Ban Ki-moon akitoa wito wake kwa pande zote kusitisha mapigano mara moja na kurejelea meza ya mazungumzo mjini Cairo, Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.