Askari wa Urusi kushiriki katika mapigano nchini Syria
Askari wa Urusi wameanza kushiriki katika vita nchini Syria ili kuisaidia serikali ya Rais Bashar Al Assad, vyanzo kadhaa vya Lebanon vimearifu kutokana na hali ya kisiasa na kijeshi inayoendelea kushuhudiwa nchini humo.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa vyanzo vya Marekani, Urusi imetuma nchini Syria masaa machache yaliyopita meli mbili zilizobeba magari ya kijeshi na ndege za ziada pamoja na kikosi kidgo cha wa nchi kavu na majini.
Afisaa wa waasi wa Syria alisema awali kwamba idadi ya washauri wa kijeshi kutoka Urusi waliongezeka katika kipindi cha mwaka uliyiopita.
Kwa mujibu wa afisaa wa Marekani, Urusi huenda ikaendesha shughuli mbalimbali katika uwanja mdogo wa ndege ilio karibu na bandari ya Latakia, ngome kuu ya vikosi vinavyomuunga mkono Rais Bashar Al Assad, ambavyo vilipata hasara kubwa miezi ya hivi karibuni.
Moscow imehakikisha kuwa kuna wataalam wake wakijeshi waliotumwa katika uwanja wa mapigano, lakini imethibitisha kwamba wataalam wake hao hawashiriki katika vita. Damascus pia imethibitisha kwamba washauri wa kijeshi kutoka Urusi hawashiriki moja kwa moja katika shghuli yoyote ya kijeshi nchini Syria.
Urusi ina kambi ya jeshi la majini katika bandari ya Tartus, Urithi wa Soviet katika zama hizo.
Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya Lebanon, ambavyo havikutaka kutajwa, Urusi inajaribu kuweka kambi mbili nchini Syria, moja karibu na pwani, nyingine katika mjoa ya mikoa ya Syria.