Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza mjini Geneva

Kikao cha nne cha mazungumzo ya amani ya Syria mjini Geneva kimeanza Alhamisi hii, ambapo wawakilishi wa serikali na wale wa upinzani wanakutana ili kutafutia suluhu mgogoro naoendelea.

Mazungumzo ya amani ya Syria yanafanyika mjini Geneva chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.
Mazungumzo ya amani ya Syria yanafanyika mjini Geneva chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria alianza mashauriano na wawakilishi wa serikali ya Syria na upinzani kabla ya kuzindua rasmi mazungumzo hayo.

Vikao vitatu tayari vilifanyika mwaka 2016 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa lakini vilishindwa kuleta amani nchini Syria, ambako zaidi ya watu 310,000 wamepotza maisha na mamilioni wamekimbilia katika maeneo salama na katika nchi jirani ili kuepuka miaka sita ya vita.

Kikako cha nne cha mazungumzo ya amani kijulikanacho kwa jina la "Geneva 4" kimefunguliwa wakati ambapo waasi wa Syria wanaounga mkono Uturuki kutangaza wameukomboa mji wa Al-Bab, ngome ya mwisho ya kundi la Islamic State kaskazini mwa Syria.

Hata kabla ya kuanza kwa duru hii mpya ya mazungumzo, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa, Staffan de Mistura, alisema ana matumaini ya kupatikana kwa suluhu ya moja kwa moja katika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.