Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Yemen: Serikali na wanaharakati wanaotaka kujitenga watia saini mkataba wa amani

Vita inaendelea nchini Yemen, lakini makundi mawili hasimu katika vita hiyo yamekubali kuweka kando tofauti zao na kutia saini mkataba wa amani kwa eneo la Kusini mwa nchi hiyo.

Mkataba ulitiwa saini mbele ya wakuu kutoka nchi za Saudi Arabia Mohammed ben Salman (katikati), Falme za Kirabu, Mohammed ben Zayed (kushoto) na Rais wa Yemeni Abd Rabbo Mansour Hadi (d) Jumanne (Novemba 5) Riyadh.
Mkataba ulitiwa saini mbele ya wakuu kutoka nchi za Saudi Arabia Mohammed ben Salman (katikati), Falme za Kirabu, Mohammed ben Zayed (kushoto) na Rais wa Yemeni Abd Rabbo Mansour Hadi (d) Jumanne (Novemba 5) Riyadh. Saudi Press Agency/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wanaotaka kujitenga katika eneo la kusini mwa Yemen na serikali ya nchi hiyo wamerasimisha maridhiano yao katika sherehe ya kutia saini mkataba wa amani iliyofanyika nchini Saudi Arabia.

Mkataba huo, uliyotangazwa mwishoni mwa mwezi Oktoba, utawezesha kurudi kwa hali ya utulivu Kusini mwa Yemen. Mkataba huo pia utawezesha kuundwa kwa serikali mpya na serikali hiyo kurudi kutumika katika mji Aden, mji mkubwa wa Kusini mwa Yemen.

Mwezi Agosti mwaka huu, waasi wanaotaka kujitenga walichukua udhibiti wa mji wa Aden baada ya mapigano dhidi ya wanajeshi watiifu kwa Rais Abd Rabbo Mansour Hadi. Makundi haya mawili yalijikuta yakikabiliana katika vita mpya, kwani mpaka sasa yamekwa yakishirikiana katika vita dhidi ya waasi wa Kihouthi.

Kwa hivyo ni maridhiano ambayo yalitiwa saini Jumanne mbele ya wakuu kutoka nchi za Saudi Arabia Mohammed ben Salman na Falme za Kirabu, Mohammed ben Zayed. Wawili hao MBS na MBZ, ambao wana nguvu katika eneo hilo la mashariki ya Kati wamemaliza uhasama uliokuwa ukiathiri nchi hio mbili, kwani Riyadh ndiye msaidizi mkuu wa kambi ya vikosi vinavyomtii rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi wakati Falme za Kiarabu ukitoa msaada kwa wanaharakati wanaotaka kujitenga kusini mwa Yemen.

Mkataba uliyosainiwa Jumanne hayahusu waasi wa Houthi wa Yemen ambao bado wanadhibiti maeneo makubwa ikiwa ni pamoja na mji wa Sanaa, mji mkuu wa Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.