Pata taarifa kuu
PALESTINA-SIASA

Hamas kususia uchaguzi wa manispaa ikiwa hakutakuwa na chaguzi zingine

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu lenye silaha la Hamas, lililoko madarakani katika Ukanda wa Gaza, limetangaza Jumatano wiki hii kwamba hailitoshiriki katika uchaguzi wa manispaa uliopangwa kufanyika mwezi Desemba ikiwa rais Mahmoud Abbas pia hakuitisha uchaguzi wa wabunge na wa urais.

Kundi la wapiganaji wa Hamas ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wa Kipalestina ambayo yanadhibiti ukanda wa Gaza, eneo ambalo mara kwa mara hulitumia kukabiliana na Israel, taifa ambalo halilitambui.
Kundi la wapiganaji wa Hamas ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wa Kipalestina ambayo yanadhibiti ukanda wa Gaza, eneo ambalo mara kwa mara hulitumia kukabiliana na Israel, taifa ambalo halilitambui. SAID KHATIB AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi ya Palestina ilitangaza wikendi iliyopita kwamba uchaguzi wa manispaa utafanyika mwezi Desemba katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, kwa kusubiri Hamas kuwezesha uchaguzi huo ufanyike katika eneo hilo.

Kundi la wapiganaji wa Hamas ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wa Kipalestina ambayo yanadhibiti ukanda wa Gaza, eneo ambalo mara kwa mara hulitumia kukabiliana na Israel, taifa ambalo halilitambui.

Awali uchaguzi wa bunge la Palestina ulikuwa umepangwa ufanyike tarehe 22 Mei, wa rais tarehe 31 Julai na wa mabaraza ya miji tarehe 31 Agosti mwaka huu.

Uchaguzi huo wa wabunge ulikuwa sehemu ya juhudi za kuleta maridhiano kati ya kundi la Hamas na chama cha Fatah ambayo yangefanikisha kufikiwa makubaliano ya kuanzishwa mazungumzo mapya na Israel kuhusu suluhisho la kuundwa madola mawili kama njia ya kumaliza mzozo kati ya Israel na Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.