Pata taarifa kuu

Papa Francis awasili Bahrain, kiongozi wa kwanza wa kanisa Katoliki kuzuru ufalme wa Ghuba

Papa Francis amewasili Alhamisi, Novemba 3, nchini Bahrain kwa ziara ya siku nne, ikiwa ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa kanisa Katoliki duniani katika ufalme mdogo wa Kiislamu wa Ghuba, ziara ambayo kwa kiasi kikubwa imejikita katika mazungumzo baina ya dini, linaripoti shirika la habari la AFP.

Papa Francis anaazuru Bahrain kuanzia tarehe 3 hadi 6 Novemba. Hapa akiwa mbele ya Kanisa Kuu,  Cathedral of Our Lady of Arabia.
Papa Francis anaazuru Bahrain kuanzia tarehe 3 hadi 6 Novemba. Hapa akiwa mbele ya Kanisa Kuu, Cathedral of Our Lady of Arabia. AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis amesafiri kwa ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Fiumicino huko Roma saa 9:45 asubuhi ya Alhamisi Novemba 3 kwa safari yake ya 39 ya kitume itakayomfikisha katika Ufalme wa Bahrain. Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kanisa Katoliki duniani kuzuru nchi hii ya Ghuba ya Uajemi yenye wakaazi milioni 1.2, ambayo ina takriban Wakatoliki 80,000, wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za nje.

Baada ya safari ya saa 5, kilomita 4,228, Papa Francis aliwasili Awali katikati mwa Bahrain saa nane na dakika :36 mchana kwa saa za Roma, sawa na saa 4:36 alaasiri kwa saa za Bahrain. Kama itifaki inavyoelekeza, hatua yake ya kwanza itampeleka kwenye Kasri ya Kifalme ya Sakhir, makazi ya mtawala wa Ufalme huo, Hamad bin Isa Al Khalifa, kilomita 5 kutoka Awali katika jangwa la Sakhir, kwa sherehe ya kukaribishwa na kukutana na mamlaka, viongozi wa mashirika ya kiraia na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Bahrain. 

Safari hii ya 39 ya kitume ni fursa mpya kwa Papa Francis kusisitiza juu ya umuhimu wa mazungumzo na Uislamu: siku baada ya kuwasili kwake, Ijumaa Novemba 4, atashiriki kikao cha mazungumzo kati ya Mashariki na Magharibi, kilichoandaliwa huko Awali, kwa ushirikiano na Imam Al-Tayeb, ambaye Francis alitia saini naye kwenye Hati ya Udugu wa Kibinadamu, huko Abu Dhabi mnamo Februari 2019. Kikao hiki cha mazungumzo  kimeandaliwa na Baraza la Wazee wa Kiislamu (Muslim Council of Elders) na kinalenga kukuza kuishi pamoja duniani na udugu wa kibinadamu.

Siku mbili kabla ya kuondoka kwake, katika hafla ya Malaika wa Watakatifu Wote, Papa Francis, kwenye dirisha la Jumba la Kitume, alikumbusha kiini cha safari hii: "maelewano muhimu" kati ya Mashariki na Magharibi, "ziara yenye ishara ya mazungumzo”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.