Pata taarifa kuu

Uongozi wa Taliban waonya UN kutowahusisha katika mazungumzo ya Doha

NAIROBI – Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kwa siku ya pili hivi leo amefanya mazungumzo na  viongozi wa mataifa yenye nguvu duniani, kuhusu jinsi ya kukabiliana na viongozi wa Taliban wa Afghanistan, huku kukiwa na onyo kutoka kwa utawala wa Kabul kwamba mkutano huo unaweza kuwa usio na tija.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa hotuba baada ya mkutano wa kilele wa faragha kuhusu Afghanistan mjini Doha, Qatar, Jumanne, Mei 2, 2023.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa hotuba baada ya mkutano wa kilele wa faragha kuhusu Afghanistan mjini Doha, Qatar, Jumanne, Mei 2, 2023. AP - Lujain Jo
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanayofanyika huko Doha, Qatar, yameandaliwa na Guterres baada ya utawala wa Taliban kuwazuia wanawake kufanya kazi katika Umoja huo, na kusababisha UN kuangazia upya shughuli zake kubwa za misaada nchini Afghanistan.

Guteress amesikitika  Afghanistan ina hitaji kubwa la msaada wa binadamu na wanaotoa msaada huo kwa niaba ya umoja huo ni wanawake ambao sasa wamezuia kufanya kazi.

Wafanyikazi wetu wengi wanaotoa huduma za msaada ni raia wa Afghanistan wengi wakiwa ni wanawake,katazo lilopo la wanawake wanaotufanyia kazi na mashirika mengine,halikubaliki na linaweka maisha ya wengi hatarini. Niwe mwazi,hatutanyamazia ,ukandamizaji wa wanawake na wasichana, amesema Guterres.

Wanwake nchini humo pia hawaruhusiwi kufanya kazi katika mashirika mengine ya kiraia na baadhi ya kazi za serikali, huku wasichana wakizuiwa kusoma katika shule za sekondari na vyuo vikuu.

Nchi ambazo zimekutana kwa mazungumzo hayo ni Marekani, Urusi, China pamoja na nchi zingine 20 na mashirika mbalimbali kukiwemo wafadhili wa Ulaya na jirani Pakistan, lakini utawala wa Taliban haujahusishwa.

Mkutano wowote bila kushirikishwa kwa wawakilishi wa Taliban, ambao ni wahusika wakuu katika suala hili, mwafaka hauwezi kupatikana, amesema mkuu wa ofisi ya Taliban huko Doha, Suhail Shaheen, akiongeza kuwa wao kutoshirikishwa ni ubaguzi.

Wakati hayo yakijiri, waziri wa mambo ya nje wa Afghan, Amir Khan Muttaqi, ataongoza ujumbe kuelekea huko Islamabad mwishoni mwa wiki hii, kwa mazungumzo na viongozi kutoka Pakistan na China, imesema wizara hiyo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, lililaani kwa kauli moja kupigwa marufuku kwa wafanyakazi wake wanawake wa Afghanistan, ambayo shirika hilo linasema limetishia pakubwa juhudi zake za kuwasaidia wakazi.

Siku ya Jumamosi, makundi ya wanawake yalifanya maandamano wakihofia mkutano wa Doha unaweza kupendekeza hatua za kutambuliwa kwa utawala wa Taliban uliorejea madarakani Agosti 2021.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric mnamo Mei 1, alisema mkutano huo unaofanyika kwa siri, utajadili haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za wanawake, utawala wa Afghanistan na njia za kukabiliana na ugaidi na biashara ya dawa za kulevya.

Umoja huo kufikia Ijumaa hii, utakuwa umekamilisha kuangazia upya operesheni zake nchini Afghanistan, iwapo utaendelea kuhudumu au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.