Pata taarifa kuu

Wapalestina watakiwa kuhamia Kusini mwa Gaza, Israel yaonya

Jeshi la Israeli limeendelea kutekeleza mashambulio ya angaa katika ukanda wa Gaza, wakati huu Wapalestina wakisema wanapokea taarifa kuhamia Kusini mwa eneo hilo,  wakati huu linapojiandaa kutuma vikosi vya aradhini kuwasaka wapiganaji wa Hamas.

Wapalestina wakiangalia madhara katika ukanda wa Gaza baada ya shambulio la jeshi la Israeli
Wapalestina wakiangalia madhara katika ukanda wa Gaza baada ya shambulio la jeshi la Israeli © AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

Hii sio mara ya kwanza, kwa Israeli kutoa onyo hili kwa Wapalestina, ikisema kuwa, wale ambao hawataondoka, watachukuliwa kama watu wanaowahurumia magaidi wa Hamas.

Hata hivyo, Wapalestina wanasema kwenda êneo la Kusini ni hatari kwa sababu jeshi la Israeli linaendelea kutekeleza mashambulizi ya angaa lakini êneo hilo pia limeshambuliwa.

Wakati onyo hilo likitokea, usiku wa kuamkia leo, kundi la Hamas linasema, watu 55 wameuawa baada ya jeshi la Israeli kushambulia msikiti katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, katika ukingo wa Magharibi.

Katika hatua nyingine, malori 20 yaliyobeba misaada ya kibinadamu kama chakula na maji, yaliingia Gaza êneo jana  ambalo wakaazi wake zaida ya Milioni 2, wameathiriwa na vita vinavyoendelea. Siku ya Jumapili, malori mengine 17 yakitokea nchini Misri, yameingia katika ukanda wa Gaza.

Vita vilianza tarehe 7 mwezi huu baada ya kundi la Hamas, kuingia katika ardhi ya Israeli na kuwauwa watu zaidi ya 1,400 na kuwateka wengine na kuzua mashambulio kutoka jeshi ambayo yamewauwa watu zaidi ya 4,300 mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.