Pata taarifa kuu

Bahrain yasitisha uhusiano wa kibiashara na Israel, na kumrejesha nyumbani balozi wake

Baraza la bunge la Bahrain limetangaza leo Alhamisi kusitisha uhusiano wa kiuchumi na Israel na kuwaondoa mabalozi wake kutokana na vita kati ya Israel na Hamas, ingawa serikali bado haijathibitisha uamuzi huo. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen na mwenzake wa Bahrain, Abdul Latif al-Zayani, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Manama, Septemba 4, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen na mwenzake wa Bahrain, Abdul Latif al-Zayani, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Manama, Septemba 4, 2023. AFP - MAZEN MAHDI
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa kwanza wa spika wa Bunge, Abdelnabi Salman, amethibitisha uamuzi huo kwa shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa "mzozo unaoendelea Gaza hauwezi kuvumilia ukimya." 

Ikiwa uamuzi huo utathibitishwa na serikali, itakuwa hatua ya kwanza kuchukuliwa na mmoja wa washirika wa Kiarabu wa Israel katika Ghuba. Bahrain na Israel zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2020 chini ya Makubaliano ya Abraham yaliyosimamiwa na Marekani.

Wakati huo huo serikali ya Hamas imetangaza vifo 27 katika mashambulizi ya Israel karibu na shule ya Umoja wa Mataifa

"Miili ya mashahidi 27 imepatikana, na pia kuna wengi waliojeruhiwa," msemaji wa wizara Ashraf al-Qidreh amesema. Idadi hii haikuweza kuthibitishwa mara moja. Katika picha kutoka AFPTV kunaonekana miili mingi iliyojaa damu ikiwa imelala chini mbele ya shule, ambapo watu wengi waliokimbia makazi yao kutokana na vita vinavyoendelea walikuwa wamekimbilia.

Jeshi la Israel limetangaza kifo cha Luteni Kanali Salman Habaka, 33, ambaye alikuwa anaongoza kikosi cha 53 cha mizinga. Ni afisa wa juu zaidi wa Israeli aliyekufa katika mzozo huu, na hivyo kufikisha idadi ya wanajeshi 18 waliouawa tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.