Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani amewasili nchini Israeli

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Israeli, ziara inayolenga kuangazia hatua ambazo zimechukuliwa kuwakinga raia kutokana na mashambulio yanayotokana na makabiliano kati ya wanajeshi wa Israeli na wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza.

Hii ni ziara ya tatu kwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani Mashariki ya kati tangu Hamas kuivamia Israeli
Hii ni ziara ya tatu kwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani Mashariki ya kati tangu Hamas kuivamia Israeli REUTERS - JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya pili kwa waziri huyo mashariki ya kati tangu wapiganaji wa Kipalestina Hamas kutekeleza shambulio kusini mwa Israeli tarehe saba ya mwezi Oktoba, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,400 wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida kwa mujibu wa maofisa wa Israeli.

Israeli kwa upande ilitekeleza shambuliuo la kujibu mapigo ya Hamas katika ukanda wa Gaza, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tisa wakiwemo zaidi ya watoto elfu tatu kwa mujibu wa wizara ya afya katika ukanda wa Gaza inyoongozwa na Hamas.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani  Antony Blinken, amewasili jijini Tel-Aviv
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, amewasili jijini Tel-Aviv © JONATHAN ERNST / AFP

Kwa mujibu wa waziri Blinken, ziara yake inalenga kujadili hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa kuzuia madhara dhidi ya raia wa Gaza wakiwemo wanawake na watoto.

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kuunga mkono msaada wa kijeshi kwa Israeli katika vita vyake dhidi ya wapiganaji wa Hamas, akieleza pia kuguswa na mateso wanayopitia raia wa Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.