Pata taarifa kuu

Krismasi: 'Mioyo yetu jioni hii iko Bethlehemu,' Papa asema

"Mioyo wetu jioni hii iko Bethlehem," Papa Francis amesema siku ya Jumapili jioni wakati wa misa ya Krismasi wakati sherehe katika mji unaokaliwa wa Ukingo wa Magharibi zinagubikwa na vita kati ya Israel na Hamas.

Papa Francis akihutubia siku ya mkesha wa Krismasi wakati wa misa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Vatican, tarehe 24 Desemba 2023.
Papa Francis akihutubia siku ya mkesha wa Krismasi wakati wa misa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Vatican, tarehe 24 Desemba 2023. © Gregorio Borgia / AP
Matangazo ya kibiashara

"Mioyo yetu, jioni ya leo, iko Bethlehemu, ambapo mkuu wa amani bado anakataliwa na hoja isiyo faa ya vita, na mapigano ambayo, hata leo, yanamzuia kupata nafasi duniani," amesema Kiogozi wa Kanisa Katolika duniai papa kutoka Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Takriban waumini 6,500, kwa mujibu wa Vatican, wamehudhuria misa iliyoongozwa na papa mbele ya viongozi wa kidini na wanadiplomasia, huku mamia ya wengine wakiifuata kwenye skrini kubwa zilizowekwa nje ya uwanja huo.

Makao makuu ya Ukristo, mji wa Bethlehem - ambapo Kristo alizaliwa kulingana na mila - iliachwa na mahujaji mwaka huu na kufuta sherehe nyingi za Krismasi kutokana na vita.

Jumapili adhuhuri, wakati wa sala ya kila wiki ya Angelus, mkuu wa Kanisa Katoliki alitaja mzozo katika Ukanda wa Gaza ambapo jeshi la Israel lilizidisha mashambulizi yake ya anga kusini mwa eneo hilo siku ya Jumapili.

"Tuko karibu na kaka na dada zetu wanaoteseka kutokana na vita: tufikirie Palestina, Israel, Ukraine," amesema.

"Kwa hali hii ya sasa, nadhani ni muhimu kusikia sauti inayotuambia: 'tafadhali sitisheni vita, kuweni na amani zaidi. Tuko katika karne ya 21, ni jambo la kutisha", amesema Filipa Sousa, 20, mtalii kutoka Porto, ambaye alihudhuria misa katika uwanja wa St. Peter, ameliambia shirika la habari la AFP.

Papa Francis, raia Argentina atatamka baraka zake za kitamaduni za “Urbi et Orbi” (“To the city and to the world”) siku ya Jumatatu saa sita kamili mchana , ambapo kwa jadi atatoa muhtasari wa migogoro katika dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.