Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Vita Gaza: Hamas nchini Misri kujadili usitishwaji mapigano

Makubaliano ya kusitisha mapigano yanajumuisha kusitishwa kwa mashambulizi ya Israel na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina ili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka waliotekwa nyara wakati wa mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.

Wapalestina, ambao walitoroka makazi yao kwa sababu ya mashambulizi ya Israeli, wanapewa hifadhi katika kambi ya hema kwenye mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 10, 2024.
Wapalestina, ambao walitoroka makazi yao kwa sababu ya mashambulizi ya Israeli, wanapewa hifadhi katika kambi ya hema kwenye mpaka na Misri huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 10, 2024. © Mohammed Salem / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Hamas unakwenda Cairo Jumamosi hii, Mei 4, "kuendelea na majadiliano" ili "kufikia makubaliano" juu ya mapatano ya amani katika Ukanda wa Gaza na Israel, ambayo inatishia kuanzisha operesheni ya ardhini katika mji wa Rafah licha ya maonyo kutoka Washington na Umoja wa Mataifa.

"Ukweli hivi sasa ni kwamba kikwazo pekee kati ya watu wa Gaza na kusitisha mapigano ni Hamas," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema siku ya Ijumaa jioni, ambaye aliuelezea mpango wa usitishwaji vita uliopendekezwa na Israel kuwa ni "mzuri".

Katika taarifa, Hamas imesema iko katika "nafasi nzuri" ya kutafakari.

Israeli "kukomesha kabisa uchokozi"

"Kwa kuzingatia mawasiliano ya hivi karibuni na wapatanishi nchini Misri na Qatar, ujumbe wa Hamas utasafiri kwenda Cairo Jumamosi kukamilisha majadiliano," imeongeza.

Ikiwa madarakani katika Ukanda wa Gaza tangu 2007, Hamas hata hivyo "imedhamiria" kupata "kukomesha kabisa uvamizi wa Israel", "kujiondoa" kwa majeshi ya Israel na "mpango mzito wa kubadilishana" mateka Waisraeli dhidi ya wafungwa wa Kipalestina.

Afisa mkuu wa Hamas amethibitisha kuwa ujumbe huo utawasili Cairo asubuhi na utaongozwa na Khalil al-Hayya, nambari 2 wa tawi la kisiasa la kundi hili katika Ukanda wa Gaza.

Na kwa mujibu wa tovuti ya Axios, mkuu wa CIA, William Burns, aliwasili katika mji mkuu wa Misri siku ya Ijumaa jioni, ishara kwamba wakati wa maamuzi muhimu umefika baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo.

Kuachiliwa kwa mateka

Wapatanishi hao - Misri, Qatar na Marekani - wamekuwa wakisubiri kwa karibu wiki moja kwa jibu la Hamas kwa ofa mpya ya kusitisha mapigano iliyowasilishwa mwishoni mwa mwezi wa Aprili. Wajumbe wa Hamas kisha wakatangaza kwamba wanaondoka Cairo, eneo la mazungumzo ya mwisho, kwenda Qatar ili kusoma toleo hili la usitishwaji vita huku wakiahidi kurudi Misri kuwasilisha majibu yao.

Ofa hiyo ni pamoja na kusitishwa kwa mashambulizi ya Israel na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina ili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Hamas la Oktoba 7 kusini mwa Israel ambalo halijawahi kutokea ambalo lilisababisha vita.

Hali yawasiwasi yatanda Rafah

Hata hivyo, Hamas inasisitiza juu ya usitishaji vita wa uhakika, ambao Israel inakataa, huku ikisisitiza kufanya mashambulizi ya ardhini katika mji wa Rafah (kusini), ngome kuu ya mwisho ya Hamas, ambapo zaidi ya Wapalestina milioni moja wamekusanyika pamoja kuhamishwa na vurugu.

"Tutafanya kile kinachohitajika kushinda na kumshinda adui yetu, ikiwa ni pamoja na huko Rafah," Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alirudia kusema wiki hii, akithibitisha nia yake ya kuanzisha mashambulizi haya "kwa makubaliano au la" ya usitishaji vita.

Lakini Hossam Badran, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema kauli za Benjamin Netanyahu kuhusu shambulio huko Rafah "zinalenga kwa uwazi kufuta uwezekano wowote wa makubaliano."

Wakati wa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, vyanzo vya hospitali viliripoti mashambulio ya Israeli huko Rafah lakini pia katika mji jirani wa Khan Younes, ulioharibiwa baada ya operesheni ya ardhini ya Israeli na mapigano makali na Hamas.

"Umwagaji damu"

Kwa mujibu wa jarida la Wall Street Journal, ambalo linanukuu vyanzo vya Misri, Israel itatoa wiki nyingine kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, vinginevyo jeshi lake litaanzisha mashambulizi yake yaliyoahidiwa kwa wiki kadhaa katika mji wa ya Rafah, uliyoko ukingoni mwa Misri.

Marekani, mshirika mkuu wa Israel, imeeleza mara kwa mara upinzani wake kwa shambulio hili.

Kulingana na Antony Blinken, Israel haijawasilisha mpango wowote wa kuwalinda raia huko Rafah. "Kwa kukosekana kwa mpango kama huo, hatuwezi kuunga mkono operesheni kubwa ya kijeshi huko Rafah, kwa sababu uharibifu ambao utaripotiwa utakuwa zaidi ya kile kinachokubalika," alionya.

"Operesheni kubwa ya kijeshi huko Rafah inaweza kusababisha umwagaji damu," Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), pia alionya siku ya Ijumaa, ambaye anaandaa mpango wa dharura "kukabiliana na ongezeko la majeraha na vifo" katika tukio la operesheni huko Rafah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.