Pata taarifa kuu

Israeli imetuma magari kivita kwenye eneo la Rafah katika ukanda wa Gaza

Israeli imetuma magari yake ya kivita katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza, jeshi lake likiripoti kuchukua udhibiti wa mpaka na nchi ya Misri, oparesheni ambayo Umoja wa Mataifa umesema maofisa wake wamezuiwa kufikisha misaada ya kibinadamu.

Jeshi la Israeli limeripoti kuchukua udhibiti wa eneo la mpaka wa Rafah na Gaza kuelekea oparesheni zake katika mji wa Rafah
Jeshi la Israeli limeripoti kuchukua udhibiti wa eneo la mpaka wa Rafah na Gaza kuelekea oparesheni zake katika mji wa Rafah AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Oparesheni hii katika eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu waliopoteza makazi yao inakuja ikiwa imepita siku moja baada ya Israeli kuwaonya raia wa Palestina kuondoka katika eneo la Rafah kuelekea oparesheni zake za kijeshi.

Video kutoka kwa jeshi la Israeli zimeonyesha magari yake ya kivita yakiwa na bendera za nchi hiyo yakipita katika eneo hilo.

Soma piaIsrael yatangaza kuwahamisha takriban watu 100,000 kutoka mashariki mwa Rafah

Haya yanajiri wakati huu msemaji wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa Jens Laerke katika taarifa yake akieleza kwamba Israeli imewazuia maofisa wake kuingia katika eneo la Rafah na Kerem Shalom.

Katika hatua nyengine, wanajeshi wa Israeli wameripotiwa kutekeleza mashambulio mazito usiku wa kuamkia leo katika eneo hilo la Rafah.

Mashambulio hayo yameripotiwa kusababisha vifo vya watu 23 kwa mujibu wa hospitali ya Kuwaiti na wengine wanne kujeruhiwa kwa mujibu wa ripoti ya hospitali ya Najjar.

Israeli kwa upande wake inasema mapendekezo ya kusitishwa kwa mapigano yaliokubaliwa na Hamas hayakufikia vigezo vyake.
Israeli kwa upande wake inasema mapendekezo ya kusitishwa kwa mapigano yaliokubaliwa na Hamas hayakufikia vigezo vyake. © AP/Ismael Abu Dayyah

Makabiliano ya hivi karibuni yameripotiwa kutokea baada wanajeshi wanne wa Israeli kuuawa katika shambulio la roketi ambalo wapiganaji wa Hamas walikiri kuhusika.

Mapigano katika ukanda wa Gaza yalianza mwezi Oktoba tarehe 7 baada ya wapiganaji wa Hamas kutekeleza shambulio dhidi ya Israeli na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1,170 wengi wao wakiwa raia wa kawaida.

Soma piaGaza: Hamas yatangaza kukubali kusitisha mapigano kutoka kwa wapatanishi wa Misri na Qatar

Kutokana na shambulio hilo la Hamas, Israeli ilitekeleza mashambulio ya kulipiza kisasi katika ukanda wa Gaza ambapo watu zaidi ya elfu 34,789 wameuwa katika eneo hilo kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya inayoongozwa na wapiganaji wa Hamas.

Misri inayopakana na Rafah ina makubaliano ya amani na nchi ya Israeli na Qatar na viongozi wa mataifa hayo wamekuwa mstari wa mbele katika kutafuta suluhu ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.