Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa: Watu 80,000 wametoroka Rafah tangu Israel iimarishe operesheni zake Mei 6

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina limesema Alhamisi kwamba takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, tangu Mei 6, wakati Israel ilipoamuru Wapalestina wanaoishi katika mji huo wa mashariki kuhama.

Palestinian children sit next to the site of an Israeli strike on a house, amid the ongoing conflict between Israel and the Palestinian Islamist group Hamas, in Rafah, in the southern Gaza Strip, Apr
Uharibifu uliofanywa na jeshi la Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 21, 2024. REUTERS - Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

"Tangu vikosi vya Israel vilipoimarisha operesheni zao Mei 6, karibu watu 80,000 wametoroka Rafah, kutafuta hifadhi mahali pengine. Mateso ambayo familia hizi hupata haywezi kuvumilika," inasema UNRWA kwenye X, ikibainisha kuwa "hakuna mahali palipo salama" katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni 1.4 wamejazana mjini Rafah, wakirejea kwenye mpaka wa Misri, wakiwemo zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao waliosukumwa kwenda katika eneo hilo na mapigano ya miezi saba na milipuko ya mabomu ambayo yameifanya kuwa magofu kaskazini kisha katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Siku ya Jumatatu, jeshi la Israel liliwaamuru wakaazi wa vitongoji vya mashariki mwa Rafah kuhama kabla ya kuzidisha mashambulizi yake ya mabomu kwenye maeneo haya na kufanya uvamizi wa ardhini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.