Pata taarifa kuu

Guterres: Mashambulizi ya ardhini ya Israel huko Rafah yatasababisha 'janga kubwa la kibinadamu,'

Mashambulizi ya ardhini ya Israel huko Rafah yatasababisha "janga kubwa la kibinadamu", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya siku ya Ijumaa, baada ya wapatanishi kutoka Israel na Hamas kumaliza mazungumzo ya usitishaji Β vita Cairo bila makubaliano.Β 

Moshi unaongezeka kufuatia mashambulizi ya Israel, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas, Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza Mei 6, 2024.
Moshi unaongezeka kufuatia mashambulizi ya Israel, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas, Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza Mei 6, 2024. Β© Hatem Khaled / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Tumejikubalisha kikamilifu na pande zote zinazohusika ili kurejesha upatikanaji wa vifaa muhimu - ikiwa ni pamoja na mafuta yanayohitajika - kupitia vivuko vya Rafah na Kerem Shalom," ameongeza Antonio Guterres, wakati wa ziara yake mjini Nairobi, akiongeza kuwa Ukanda wa Gaza unakaribia kukumbwa na njaa.

Wakati huo huo Israel imeripotiwa kutekeleza mashambulio mpya katika ukanda wa Gaza, hatua inayokuja baada ya wapatanishi wa mzozo unaoendelea mashariki ya kati kuondoka mjini Cairo bila ya kuafikia makubaliano.

Mashambulio haya ya mapema leo Ijumaa, yanakuja wakati huu ambapo Misri nchi mojawapo wa wapatanishi wa mzozo wa Gaza, ikisema ni lazima Hamas na Israeli walegeze misimamo iwapo wanahitaji kuafikia suluhu la kusitisha mapigano pamoja na kubadilishana wafungwa.

Mapigano kati ya pande hizo mbili yameingia Β katika mwezi wa saba sasa licha ya wito wa jamii ya kimataifa wa kutaka muafaka kuafikiwa mara moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.