Pata taarifa kuu

Raia wa Palestina zaidi ya laki moja wametoroka katika mji wa Rafah

Watu zaidi ya Laki Moja, wamekimbia kutoka kwenye mji wa Rafah, ulipo kwenye ukanda wa Gaza, kuhofia mashambulio ya jeshi la Israeli, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Watu zaidi ya Laki Moja, wamekimbia kutoka kwenye mji wa Rafah.
Watu zaidi ya Laki Moja, wamekimbia kutoka kwenye mji wa Rafah. © Ramadan Abed / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kukimbia kwa wakaazi wa Rafah, linakuja wakati huu kundi la Hamas likisema, mazungumzo na Israeli kujaribu kutafuta mkataba, yaliyokuwa yanaendelea jijini Cairo, yamekwama, na wajumbe wake wameondoka.

Aidha, viongozi wa kundi hilo wamesema baada ya mwafaka kutopatikana, hatima ya upatikanaji wa mkataba wa kusitisha vita kwenye ukanda wa Gaza, ipo mikononi mwa Israeli.

Soma piaWaelfu ya watu waendelea kuutoroka mji wa Rafah kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israel

Wanajeshi wa Israeli nao wameendelea kurusha mabomu kwenye mji wa Rafah, huku afisa wa Juu wa Umoja wa Mataifa akisema, operesheni za kutoa misaada ya kibinadamu kwa sasa imeshindikana.

Licha ya wito wa Jumuiya ya Kimataifa kuitaka Israel kutoendelea na operesheni yake mjini Rafah na hata Marekani kusema haitotuma silaha kusaidia operesheni hiyo, kwa hofu ya kuwauwa rais wasiokuwa na hatia.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, nchi yake itasimama peke yake, hata kama haitopokea msaada wa nje, na kusisitiza kuwa itaendelea na mpango wake wa kuishambulia Rafah.

Katika hatua nyengine katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio katika makao makuu wa shirika la UN kuhusu wakimbizi wa Palestina UNRWA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.