Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa Uturuki atangaza kuiachiya ngazi iwapo chama chake kitashindwa kwenyea mitaa

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema jumatano kuwa yupo tayari kuachia madaraka ikiwa chama chake ambacho kinatawala kwa sasa kikishindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Waziri m,kuu wa Uturuki Recep Tayep Erdogan
Waziri m,kuu wa Uturuki Recep Tayep Erdogan REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Erdogan ambaye anakabiliwa na tuhuma za ufisadi ambazo zimemletea changamoto katika utawala wake wa miaka 11 amesema yupo tayari kuondoka mamlakani vinginevyo chama chake kifanye vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa zilizopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi huu.

Hata hivyo upinzani wameshambulia kauli ya Erdogan kwa kuona ni matamshi ya ya kisiasa ambayo yamejawa na dharau.

Naibu mkuu wa chama cha MHP Mehmet Sandir, amesema matamshi ya Erdogan ni sawa na kuteka matakwa ya watu na kutoiheshimu jamii kwa kuonesha jamii kuwa wanapiga kura kwa ajili ya Erdogan.

Serikali ya Erdogan inakabiliw ana shinikizo kutoka kwa upinzani ambao unamtaka kujiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa, hatuwa iliopelekea mawaziri kadhaa wa serikali kujiuzulu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.