Pata taarifa kuu
AFRIKA-ULAYA

Mkutano kati ya viongozi wa Afrika na Ulaya waanza Brussels

Viongozi wa Afrika na wenzao kutoka barani Ulaya wanakutana mjini Brussles nchini ublegiji leo na kesho kujaidli maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya mabara hayo mawili, kiuchumi na kidiplomasia.

Rais wa Madagascar, Rajaonarimampianina akiwasili Brussels kushiriki mkutano kati ya viongozi wa Afrika na Umoja wa Ulaya.
Rais wa Madagascar, Rajaonarimampianina akiwasili Brussels kushiriki mkutano kati ya viongozi wa Afrika na Umoja wa Ulaya. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unaolenga masuala ya kiusalama, maendeleo ya kiuchumi na uhamiaji utatanguliwa mkutano wa awali kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati akiwepo Rais wa Ufaransa François Hollande na rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati bi Catherine Samba Panza.

Viongozi wapatao 80 wa Afrika na Ulaya wanatarajiwa kuwepo hii leo mjini humo kujaribu kufufua ushirikiano wao na kukosekana kwa utulivu barani Afrika pamoja na kupoteza ubia wa dhati kufwatia ushindani wa Kichina.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon naye anatarajiwa kuwasili katika mkutano huo muhimu ambapo migogoro baada ya ukoloni inaonekana kudhoofisha maendeleo jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya viongozi wa Afrika kama Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye ameamua kususia mkutano huo kwa ukosefu wa visa kwa mkewe Grace Mugabe.

Lengo la mkutano huo ni kutoa msaada katika maeneo kadhaa ikiwemo masuala ya usalama , haki za binadamu pamoja na Ushirikiano.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni kuwekeza kwa watu kwa ajili ya ustwai na amani. Lakini miongoni mwa maswala yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na mzozo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, vitendo vya kigaidi barani Afrika.

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Ulaya umefahamisha jana kwamba umeanzisha operesheni ya kijeshi. Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa wapatao 2000 na wale 6000 wa Umoja wa Afrika walitumwa kusimamia amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, raia wa waishiyo katika mitaa ya kaskazini wanaendelea kukimbilia kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani, baada ya vifo vya watu 24 waliyouawa na wanajeshi kutoka Chad mwishoni mwa juma katika mazingira ya kutatanisha.

Suala la wahamiaji haramu barani Afrika ni miongoni mwa maswala tata yatakayojadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir hakualikuwa katika mkutano huo kwa sababu anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, naye rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesusia mkutano huo baada ya mkewe kunyimwa viza ya kwenda Ulaya.Katika hali hiyo, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesitisha kuwasili kwake katika mkutano huo, lakini ametuma wawakilishi wake kwa kile alichokieleza kuwa sio vizuri kuhudhuria mkutano huo bila ya kuwepo kwa rais Mugabe amabye ni mshirika wake wa Karibu.

Marais wa Angola na Swaziland wakisubiriwa kuthibitisha kuwepo kwao katika mkutano huo.

Naye rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, hatakuwepo lakini ametuma wawakilishi wake kwa kile alichokieleza kuwa sio vizuri kuhudhuria mkutano huo bila ya kuwepo kwa rais Mugabe amabye ni mshirika wake wa Karibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.