Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-NATO

Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi Nato yasitisha ushirikano wake na Urusi

Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi Nato, imesitisha ushirikiano wake na Urusi katika masuala ya kiraia na kijeshi, kutokana na nchi hiyo kuingilia katika masuala ya Ukraine, huku Urusi ukipewa nafasi katika mazungumzo katika hali ya kupatia ufumbuzi mgogoro wa Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague akiwa pamoja na katibu mkuu Umoja wa kujihami wa mataifa ya magharibi NATO, Anders Fogh Rasmussen (kulia).
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague akiwa pamoja na katibu mkuu Umoja wa kujihami wa mataifa ya magharibi NATO, Anders Fogh Rasmussen (kulia). REUTERS/Laurent Dubrule
Matangazo ya kibiashara

Baada ya majuma kadhaa ya mvutano baina ya mataifa mbalimbali jana jioni, bunge la Marekani limeidhinisha mpango wa kuisaidia Ukraine na kuichukulia vikwazo Urusi.

Mpango huo unalenga kuipatishia msaada serikali ya Kiev hadi kufikia kiwango cha dola bilioni moja, ambao utasaidia Ukraine kujiimarisha kiuchumi ili “kuipa nafasi nchi hio kujidhatiti kimaendeleo”, amesema rais wa Marekani Barack Obama.

Mawaziri 28 wa mambo ya nje kutoka mataifa wanachama wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi NATO wamechukuwa uamzi wa kusitisha ushirikiano wao na Urusi katika masuala ya kiraia na kijeshi, amesema katibu mkuu wa jumuiya hio Anders Fogh Rasmussen.

Nato na Urusi vinashirikiana pia na mataifa ya ulimwengu wa tatu katika masuala ya kupambana na maharamia katika bahari ya Hindi pamoja na ugaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amejizuiya kutoa taarifa yoyote, akibaini kwamba hakutaka hali hio izidi kuleta mvutano.

Wakati huu, mataifa vigogo ya Ulaya ya masariki wameamua kutekeleza uamzi huo uliyochukuliwa majuma kadhaa yaliyopita, ikiwa ni pamoja na kutuma kwa muda ndege za ukaguzi aina ya Awacs za NATO pamoja na ndege nyingine za Marekani aina ya F-15 na F-16 katika mataifa ya Lithuania naPoland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.