Pata taarifa kuu
Ukraine-Urusi-diplomasia

Urusi na Ukraine zajadiliana juu ya swala la gesi

Taarifa kutoka Kamishna ya Umoja wa Umoja wa Ulaya imefahamisha kuwa mazungumzo kati ya pande tatu hususan Urusi, Ukraine na Umoja wa Ulaya juu ya Urusi kuendelea kutowa huduma ya gesi kwa Ukraine na kumaliza tatizo la malimbikizo ya madeni yameanza hii leo jijini Brusels.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov Le Parisien
Matangazo ya kibiashara

Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na maswal ya nishati Günther Oettinger pamoja na mawaziri wa Urusi na Ukraine wa nishati Alexandre Novak na Iouri Prodan, wanakutana katika mazungumzo ambayo yanataraji kuchukuwa muda wa siku nzima na ambayo yanafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya, wajumbe wa makampuni ya Urusi ya nishati Gazprom na Ukraine Naftogaz wanahudhuria pia.

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, waziri mkuu wa Ukraine Arsene Iatseniouk amesema katika kikao cha baraza la mawaziri kuwa serikali yake imetupilia mbali pendekezo la Urusi la kupunguza takriban dola mia moja katiba beo iliopangwa ambayo ilitoka kwenye 268 hadi 485 tangu April Mosi mwaka huu

waziri huyo amesema wanautambuwa mtengo wa Urusi, kupunguza kwa bei ya gesi kumeamuliwa na serikali na kuondolewa kwa uamuzi huo kunaweza pia kuamuliwa na serikali, na hivo mapendekezo yao yatasalia kuwa walivyowasilisha na ambapo mkataba lazima ubadilishwe.

Pendekezo la serikali ya Kiev ni kutozwa bei inayo kubalika katika masoko barani ulaya. Pande hizo mbili zinakutana kujaribu kumaliza taofauti hiyo ambayo inaweza kupelekea Urusi kukata huduma yake ya gez kwa serikali ya Kiev hatuwa ambayo inaweza pia kuvurugu utowaji wa huduma kwa mataifa mengine barani Ulaya.

Shirika la Gazprom limesisitiza juu ya Ukraine kulipa madeni yake ambayo yamefikia dola za Marekani Bilioni 4.5 na kutishia kutumia mfumo wa malipo kabla, iwapo madeni hayo hayatolipwa, jambo ambalo linaweza kusababishwa kukatiwa kwa huduma hiyo. Serikali ya Urusi imetowa muda wa hadi Juni 16 madeni hayo yawe tayari yamelipwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.