Pata taarifa kuu
Iraq-waasi

Watu 48 watekwa wakati huu wapiganaji wa kijihadi wakitishia kuendeleza mapambano zaidi nchini Iraq

Kundi la wapiganaji wa Kijihadi nchini Iraq limetishia kuendeleza mapigano zaidi baada ya kufaulu kuyateka maeneo kadhaa yenye wafuasi wengi waumini wa Kisuni kaskazini mwa nchi hiyo wakati huu jeshi dhaifu la Iraq likitimka, hali ambayo iliosababisha wakaazi wengi wa Mosoul kuyahama makwao. Hayo yanajiri wakati huu watu 48 wakitekwa katika ubalozi mdogo wa Uturuki mjini Mosoul, na ambapo matrka wote ni raia wa Uturuki.

wapiganaji wa kijihadi walioiteka miji kadhaa nchini Iraq
wapiganaji wa kijihadi walioiteka miji kadhaa nchini Iraq trt
Matangazo ya kibiashara

Wataalamu wa maswala ya kijeshi wanaonakuwa hatuwa ya wapiganaji wa makundi ya kijihadi nchini Iraq kuuteka mji mwingine nchini Iraq na vitongoji vingi kaskazini mwa nchi hiyo huenda wapiganaji hao wakatekeleza azma yao ya kuunda taifa la Kiislam katika eneo hilo lenye mpaka kati ya Syria na Iraq.

Kundi la EIIL limejigamba kuhusika katika mashambulio tofauti kwenye eneo hilo, hali inayo dhihirisha udhaifu wa vikosi vya serikali ya Iraq ambavyo vitakuwa na kibarua kigumu kurejesha kwenye himaya ya serikali maeneo hayo.

Waziri mkuu wa Iraq Nuri Al Maliki ameliomba bunge la nchi kutangaza hali ya hatari katika miji iliotekwa na waasi hao wakati huu wakitangazwa kuuteka mji wa Tikrit na sasa wanaelekea  katika mji mkuu Bagdad

Wapiganaji hao wamevamia mji wa Mossoul jana jumanne na eneo zima la mji wa Ninive ambako vikosi vya usalama viliamuwa kutimka na kuacha sare zao na magari, wakati wapiganani hao walipokuwa wakisonga mbele kwenye uwanja wa mapambano ambapo walifaulu pia kuteka miji ya Kirkouk na Salaheddine.

Kuanguka kswa mji wa Ninive ni hatuwa ambayo inawapa nafasi waasi kuw ana mawasiliano na eneo la Anbar na Mosoul mpakani na Syria ambapo watasafirisha silaha zao kiurahisi na ufadhili wa wapiganaji katika vituo mbalimbali.

Mji wa Anbar kusini mwa Ninive kwenye mpaka na Syria upo mikonini mwa wapiganaji waasi wa serikali, wakati wapiganai wa kijihadi wakifaulu kuiteka miji kadhaa upande wa mashariki.

Kundi la EIIL linalenga kuiteka miji kadhaa ili kuunda taifa la kiislam lenye kutumia mfumo wa Sheria za Kiislam na kupanga mashambulizi ili kuendeleza mapambano. Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yamerahisisha azama hiyo ya wapiganiji wa kijihadi na ambapo wafuasi wake sasa wanaona kuwa lengo la kundi hilo linawezekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.