Pata taarifa kuu
Urusi-Ukraine

Urusi yaituhumu Ukraine kutumia silaha zilizopigwa marufuku

Nchi ya Urusi imetuhumu serikali ya Ukraine kwa madai kuwa vikosi vyake vinatumia silaha ambazo zimepigwa marufuku wakati huu ikijaribu kurejesha kwenye himaya yake miji inayoshikiliwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.

Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Urusi
Matangazo ya kibiashara

Tuhuma hizi zimetolewa na wizara inayohusika na haki za binadamu ya Urusi, ambapo imesema kuwa majeshi ya Ukraine yamekuwa yakitumia aina ya mabomu ambayo yamepigwa marufuku kutumiks kwenye mapambano chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa haki za binadamu nchini Ukraine, Konstantin Dolgov amewaambia wanahabari mjini Moscow kuwa, vikosi vya Kiev vimekuwa vikitumia mabomu yanayokatazwa kwenye uwanja wa mapambano kuwakabili wapiganaji wenye silaha na raia kwenye mji wa Slavyansk.

Wizara ya afya nchini Ukraine imesema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na mapigano ya mashariki mwa nchi hiyo imefikia watu 270 ikujumuisha wapiganaji wenye silaha, raia na wanajeshi wa Serikali.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov amesema kuwa hakuna maendeleo yoyote yaliyofikiwa kati yake na utawala wa Kiev katika kufikia suluhu ya mzozo wa mashariki mwa nchi hiyo, katika kile waziri Lavrov anasema kuwa ni kutokana na kushtushwa na taarifa kuwa vikosi vya Ukraine vinatumia silaha zilizokatazwa kutumiwa kwenye uwanja wa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.