Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UNICEF-Haki za binadamu

Uingereza : mkutano kuhusu kupiga vita ndoa za kulazimishwa waanza

Zaidi ya wanawake milioni 700 duniani waliolewa wakiwa bado ni watoto, shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya watoto Unicef limefahamisha, wakati likiandaa jumanne wiki hii mjini London mkutano kuhusu kupiga vita ndoa za kulazimishwa pamoja na tabia ya ukeketaji.

Wanawake wengi duniani waolewa wakiwa na umri mdogo.
Wanawake wengi duniani waolewa wakiwa na umri mdogo. RFI/Laurent Correau
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ambao unajulikana kwa jina la “Girl Summit 2014” ikimaanisha mkutano kuhusu wasichana mwaka 2014, unaandaliwa kwa ushirikiano na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, na ni mkutano wa kwanza wa aina hio kuandaliwa , Unicef imesema.

Lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kushawishi watu ili ndoa za kulazimishwa pamoja na tabia ya ukeketaji, ambayo inawakabili wanawake na wasichana milioni 130 duniani, vikomeshwe.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, wanawake milioni 250 miongoni mwa wanawake milioni 700 waliolewa wakiwa na umri uliyo chini ya miaka 15.

Hayo yakijiri tabia ya ukeketaji inashuhudiwa hasa katika nchi 29 za bara la Afrika na mashariki ya Kati. Unicef imebaini kwamba kwa sasa watu wengi wameanza kuachana na tabiya hiyo ya ukeketaji, huku ikisema kwamba athari ya ukeketaji imepungua kwa theluthi moja kwa msichana anaetimiza umri wa miaka 30.

“Lakini iwapo hakutochukuliwa hatua maridhawa na kuzidisha juhudi kwa wadau wote, mamia ya mamilioni ya wasichana wanakabiliwa na athari juu ya ukeketaji, imeonya Unicef.

Le gouvernement britannique doit annoncer dans la journée une nouvelle législation afin de poursuivre au Royaume-Uni les parents qui n'empêchent pas leur fille d'être excisée.
Serikali ya Uingereza itatangaza jumanne hii jioni sheria mpya itakayowafuatilia wazazi ambao hawawakatazi wasichana wao kujihusisha na tabia ya ukeketaji.

Manzoni mwa mwezi wa Juni, ripoti ya bunge la Uingereza lilitaja tabia hio kwamba ni “athari inayolikabili taifa”, baada ya viongozi wa Uingereza kushindwa kupambana dhidi ya tabia ya ukeketaji, ambayo inawagusa wanawake 170.000 nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.