Pata taarifa kuu
EU-UKRAINE-URUSI-Vikwazo-Diplomasia

EU: Ukraine: Urusi yachukuliwa vikwazo vipya

Makubaliano ya kusitishwa mapigano nchini Ukraine yameendelea kutekelezwa, licha ya hali ya wasiwasi kuendelea kuripotiwa katika miji ya Donetsk et Marioupol. Wafungwa 650 wameachiliwa huru jumatatu wiki hii.

Rais wa Ukraine,Petro Porochenko, akikagua jeshi lake, mjini Marioupol, Septemba 8 mwaka 2014.
Rais wa Ukraine,Petro Porochenko, akikagua jeshi lake, mjini Marioupol, Septemba 8 mwaka 2014. REUTERS/Mykola Lazarenko/Ukrainian Presidential Press Service/Ha
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, rais wa Ukraine Petro Porochenko ameifanya ziara ya kushtukiza katika mji wa Marioupol, mji uliyo karibu na bahari ya Azov, ambao umekua ukishuhudia vitisho kutoka kwa waasi. Rais Porochenko akiwa mjini Marioupol, ameongea kwa sim na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Umoja wa Ulaya (EU), ambao bado ina hofu juu ya mkataba huo, umeidhinisha walikubaliana jana jumatatu wiki hii, vikwazo vipya dhidi ya Urusi. Hata hivyo, Umoja huo wa Ulaya umeipa muda Urusi ili iweze kujirekebisha, kwani vikwazo hivyo vitaanza kutekelezwa wakati vitakua vimechapishwa katika gazeti rasmi la Umoja wa Ulaya, mchakato ambao unaweza kuchukua siku kadhaa. Moscow imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia vikwazo hivyo vipya dhidi yake..

"Kama sekta ya nishati imewekewa vikwazo au sekta ya fedha imewekewa vikwazo vya ziada, sisi hatutosita kujibu" imeonya Moscow. Waziri Mkuu Dmitry Medvedev, ameendelea kuonekana akiwa mstari wa mbele kwa kupambana na Umoja wa ulaya na Marekani kwa vikwazo vinavyochukuliwa dhidi ya Urusi wakati ambapo Putin akionekana kutafuta mazungumzo ya amani na Rais wa Ukraine Poroshenko.

Hata hivo waziri mkuu wa Urusi, Dmitri Medvedev amepiga marufuku ndege za mataifa ya magharibi kupaa kwenye anga ya Urusi.

“ Iwapo mashirika ya ndege ya mataifa ya magharibi yataruhusu ndege zao kupaa kwenye anga ya Urusi yawe tayari kukubali chochote kitakachotokea kwa ndege zao”, ameonya Medvedev. Kwa upande wake rais wa Urusi Vladimir Putin amesema vikwazo vya Umoja wa Ulaya na marekani ni havina nguvu yoyote, lakini amekubali kuwa Urusi inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

Rais Putin ana matumaini kwamba mgogoro wa Ukraine utapatiwa ufumbuzi. “iwapo viongozi wa Ukraine waytaonesha nia nzuri, na kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Urusi”, amesema rais Putin.

Hayo yanajiri wakati jumanne wiki hii, kutatolewa ripoti ya kwanza ya uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia Airlines, iliyodunguliwa nchini Ukraine katikati ya mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.