Pata taarifa kuu
UFARANSA-PALESTINA-KURA-Haki

Wabunge wa Ufaransa wapiga kura ya kulitambua taifa la palestina

Wabunge wa Ufaransa wanatazamiwa kulipigia kura Jumanne Desemba 2 azimio linaloitolea wito serikali ya Ufaransa kulitambua taifa la Palestina.

Bunge la Ufaransa lapiga kura ya kulitambua taifa la Palestina, lakini kura hizo hazina nguvu ya kubadili msimamo wa serikali ya Ufaransa.
Bunge la Ufaransa lapiga kura ya kulitambua taifa la Palestina, lakini kura hizo hazina nguvu ya kubadili msimamo wa serikali ya Ufaransa. REUTERS/Jacky Naegelen
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo liliyopendekezwa na Wasochialisti litapitishwa, lakini litakua halina nguvu yoyote kwa serikali ya Ufaransa, kwani ni kura ya ishara, kuonesha kuwa Bunge la Ufaransa linaitambua taifa la palestina.

Kura hiyo ya ishara haitobadili msimamo rasmi wa Ufaransa. Vikao kama hivyo vya Bunge vimekua vikifanyika katika nchi nyingi barani Ulaya na kupitisha uamzi wa kulitambua taifa la palestina, hali ambayo imekua ikiwapa motisha na faraja raia wa Palestina.

Pendekezo hilo la azimio ambalo lilitolewa na Wasochialisti lilijadiliwa na Bunge Ijumaa Novemba 28 mwaka 2014. Pendekezo hilo liliitolea wito serikali ya Ufaransa kulitambua taifa la Palestina. Serikali ya Ufaransa, inabaini kwamba muda haujawadia Palestina kuwa taifa. Ufaransa inaona kwamba mazungumzo kati ya Israel na Palestina ndiyo yatapelekea kuundwa kwa taifa la Palestina.
Jitihada za Wabunge na Maseneta wa Ufaransa ni ishara yenye nguvu kwa jumuiya ya kimataifa.

Qassem Barghouti, mwanae kiongozi wa mamlaka ya Palestina, alibaini hivi karibuni kwamba jitihada za Wabunge wa Ufaransa hazitobadili chochote msimamo wa serikali ya Ufaransa.

“ Nadhani kwamba jitihada hizi zinazofanywa na Wabunge wa Ufaransa na wale kutoka nchi mbalimbali za Ulaya, ni muhimu na zinawafariji raia wa Palestina kwamba wabunge kutoka mataifa mbalimbali barani Ulaya wanawaunga mkono, kwa sababu katika kila nchi, Bunge linawakilisha raia”, alisema Qassem Barghouti.

Hivi karibuni Sweden ilichukua uamzi wa kulitambua taifa la Palestina. Sweden ni nchi ya kwanza barani Ulaya kulitambua taifa la palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.