Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-Maandamano

Maandamano ya kitaifa: siku ya furaha kwa Hollande

Baada ya siku tano Ufaransa ikiwa katika hozuni na majonzi kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyogharimu maisha ya watu 12 mjini Paris, hatimaye rais François Hollande amekua ni mwenye furaha Jumapili Januari 11.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na François Hollande, Desemba 11 mwaka 2015 katika Ikulu ya Paris.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na François Hollande, Desemba 11 mwaka 2015 katika Ikulu ya Paris. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Rais Hollande akiwa na marais wengine wakigeni pamoja na viongozi wa serikali na mamia kwa maelfu ya raia waliandamana jana Jumapili kwa heshi ya waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katikati ya juma lililopita mjini Paris na vitongoji vyake.

Watu kati ya milioni 1.3 na milioni 1.5 waliandamana katika mji mkuu wa Ufaransa Paris.

Takribani viongozi 56, ikiwa ni pamoja na marais 44 wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na Ulaya, wamekutana Jumapili Januari 11 mjini Paris kwa kuonesha umoja wao.

Wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na rais wa sasa na mtangulizi wake, walijiunga na mamia ya maelfu ya raia, na kuandamana katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.