Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UCHAGUZI-SIASA

Chama cha Syriza chashinda uchaguzi wa bunge

Chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza nchini Ugiriki kinatazamiwa kuunda serikali hivi karibuni baada ya kushinda uchaguzi wa Wabunge.  

Kiongozi wa chama cha Syriza, Alexis Tsipras, baada ya kutangazwa ushindi wa chama chake, Jumapili, Januari 25 mjini Athènes.
Kiongozi wa chama cha Syriza, Alexis Tsipras, baada ya kutangazwa ushindi wa chama chake, Jumapili, Januari 25 mjini Athènes. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Chama hicho kinadaiwa kupata zaidi ya asilimia 36 ya kura dhidi ya chini ya asilimia 28 ya vyama vya kihafidhina, licha ya kuwa matokeo bado ni ya awali.

Chama hicho cha Syriza kinchoongozwa na Alexis Tsipras, kimekosa viti vya kutosha Bungeni kuweza kuongoza serikali. Hata hivyo serikali inaweza kuundwa Jumatano wiki hii.

Chama hicho cha Syriza kimekua kikipinga hatua ya kubana matumizi nchini Ugiriki. Kiongozi wa chama cha Syriza, Alexis Tsipras, amewaambia wafuasi wake katika mji mkuu wa Ugiriki, Anthens kuwa hatua ya kubana matumizi iliyotangazwa na serikali inayoondoka madarakani, imefikia mwisho na watafanya kazi na wakopeshaji na kukubaliana namna ya kushughulikia madeni ya taifa.

Waziri mkuu anayeondoka madarakani Antonis Samaras amemtaka kiongozi wa chama cha Syriza Alexis Tsipras kumpongeza. Samaras anadai kuwa sera zake zilisaidia kufufua uchumi wa Ugiriki na kwamba walichukua hatua kudumisha hali ya usalama wa raia. Amesema kuwa anakabidhi nchi ambayo ni mwanachama wa umoja wa Ulaya na sarafu ya euro.

" Raia wa Ugiriki wameandika historia", amesema kiongozi wa Syriza, Alexis Tsipras, jioni ya ushindi wa chama chake katika uchaguziwa Wabunge. Mbele ya maelfu ya wafuasi walikusanyika kwenye ukumbi wa chuo Kikuu cha Athens, Alexis Tsipras alitangaza " mwisho wa utumwa" na "ishara muhimu kwa Ulaya, ambayo inabadilika".

Hata hivyo, alionya kuwa serikali ya Ugiriki itakuwa " tayari kushirikiana na kujadili na wakopeshaji [wake] kwa ajili tu ya ufumbuzi na manufaa kwa kila mtu".

" Hakuna mshindi au aliyeshindwa", amesema kiongozi wa chama cha Syriza, huku akibaini kwamba mgogoro unaoshuhudiwa utapaswa kuupewa kipaumbele kwa kutafutiwa ufumbuzi, hususan kupiga vita rushwa na kuwatendea haki raia wote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.