Pata taarifa kuu
DENMARAK-SHAMBULIO-USALAMA

Denmark na Ufaransa zaongoza kwa wanajihadi

Vikosi vya usalama vya Denmark, Jumapili Februari 15, vimeendelea na operesheni dhidi ya makundi ya kiislam yenye silaha, baada ya kutokea kwa mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Copenhagen.

Polisi ya Denmark inayohusika na masuala ya sayansi katika eneo la mashambulizi, kituo cha utamaduni cha Krudttønden . Copenhagen, Februari 15 mwaka 2015.
Polisi ya Denmark inayohusika na masuala ya sayansi katika eneo la mashambulizi, kituo cha utamaduni cha Krudttønden . Copenhagen, Februari 15 mwaka 2015. REUTERS/Liselotte Sabroe/Scanpix Denmark
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo imemalizika mapema leo Jumapili asubuhi, wakati polisi ya Denmark ilipomuua mshukiwa mmoja wa mashambulizi hayo. Maeneo mawili yalilengwa katika mashamblizi hayo, ambayo yamekumbusha matukio ya kutisha ya mwezi uliopita katika mji wa Paris. Kama Ufaransa, Denmark, imekua ni kituo cha kuajiri wanajihadi barani Ulaya.

Ufaransa ni moja ya nchi za Ulaya ambayo ina idadi kubwa ya raia wake ambao wamejiumga na makundi ya kiislamu yenye silaha.

Inasadikiwa kuwa raia takribani 400 wa Ufaransa wamejiunga na makundi ya kiislamu yenye sialaha.

Lakini serikali ya Ufaransa inabaini kwamba wapiganaji 200 ambao ni raia wa Ufaransa waliojiunga na makundi hayo wamerejea kutoka maeneo ya mapigano.

Kwa jumla, karibu raia 600 wa Ufaransa wako au walikua nchini Syria na Iraq. Ufaransa inaongoza kwa idadi kubwa ya raia wake ambao wamejiunga na makundi ya kiislamu yenye silaha, mbele ya Uingereza na Ujerumani.

Lakini kama inalinganishwa takwimu hizi kwa wakazi wa nchi, idadi hii inabadilika kwa kiasi fulani. Kwa wakati huu Ufaransa inachukua nafasi ya tatu, nyuma ya Ubelgiji na Denmark.

Kulingana na vyombo vya kijasusi vya Denmark, zaidi ya raia 100 wa Denmark wanadhaniwa kuwa walijiunga na makundi ya kiislamu yenye silaha, ikiwa ni sawa na watu 17 kwa wakazi milioni moja. Uwiano ambao umepunguzwa kwa watu 11 nchini Ufaransa Ufaransa.

Denmark ilikuwa inaelewa kutokea kwa tishio hilo

Polisi wa Scandinavia walikuwa wanafahamu kutokea kwa tishio hilo tangu zichapishwe katuni za mtume Mohammed. Mwezi Septemba mwaka 2005, jarida la kila siku la Jyllands-staten Posten lilichapisha katuni kumi nambili ambazo zilizua hisia kubwa kwa jamii ya Waislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.