Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-UFARANSA-URUSI-CHINA-UJERUMANI-UINGEREZA-NYUKLIA-DIPLOMASIA

Mkutano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kufanyika leo

Baada ya miezi 20 ya mazungumzo, na baada ya muda wa mwisho kutamatika Jumaane Juni 30, mikutano imeendelea katika mji wa Vienna kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kabala ya kuroa msimamo wa Marekani mbele ya vyombo vya habari katika mji wa Vienna, kuhusu mpango wa nyuklia wa Marekani.
John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kabala ya kuroa msimamo wa Marekani mbele ya vyombo vya habari katika mji wa Vienna, kuhusu mpango wa nyuklia wa Marekani. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo makubwa kufanyika Jumatano wiki hii, huenda hatua ikapigwa leo jioni katika mkutano uliyopangwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano zenye nguvu duniani na Iran.

Wahusika katika Mazungumzo hayo kutoka nchi mbalimbali wanaendelea kuzungumza hadi kukabiliana na vizuizi ambavyo haviwezi kuepukika kwa upande wao. Mawaziri wa mambo ya nje, ambao wana uwezo wa kuchukua maamuzi, wamefikia sasa katika hatua ya kuvunja ukimya wao.

Hii itatokea tena siku ya Alhamisi jioni, katika mkutano ambao watashiriki waziri wa mambo ya nje wa Iran na karibu mawaziri wote wa mambo ya nje wa nchi tano kujumlisha moja (zenye nguvu duniani). Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Uingereza, China, Ufaransa na Ujerumani wanatarajiwa kushiriki mkutano huu. Urusi pekee ndio bado haijatangaza kuwasili kwa waziri wake, Sergei Lavrov.

“ Muda wa mwisho” kupangwa upya Julai 7

Kwa ujumla, mazungumzo, ambayo yanapaswa kufikia makubaliano yatakayo weka mpango wa nyuklia wa Iran chini ya usimamizi wa kimataifa ili Iran iweze kuodolewa vikwazo. Hata kama mafanikio yamepatikana, kila upande unataka kupata makubaliano ya kudumu. Hii pia, ni kuthibitisha kuwa mazungumzo ambayo yalifanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita yamekua ya kweli na yenye kuaminika.

" Bado hatujafikia hatua hiyo", amebainisha, hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier. Laurent Fabius, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa anatazamiwa kuwasili leo Alhamisi mjini Vienna ana mtazamo kama huo, ambapo ameeleza kuwa bado kuna vizuizi, lakini ana matumaini ya " kuendeleza hali hiyo."

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ameridhishwa na sentensi akisema: " Nina matumaini. "

Wakati muda wa mwisho wa tarehe 30 Juni mwaka 2015 uliahirishwa, washiriki katika mazungumzo hayo wamepanga hadi kufikia Julai 7 wawe wamefikia kwenye mkataba wa kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.