Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-SHAMBULIO-USALAMA

Uturuki: shambulio lawaua watu kadhaa Suruç karibu na mpaka wa Syria

Mlipuko mkali uliotekelezwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga umesababisha maafa makubwa leo Jumatatu mchana katika mji wa Suruç nchini Uturuki, karibu na mpaka wa Syria.

Mlipuko wasasabisha maafa makubwa Suruç, Syria, Jumatatu Julai 20 mwaka 2015.
Mlipuko wasasabisha maafa makubwa Suruç, Syria, Jumatatu Julai 20 mwaka 2015. AFP PHOTO / DICLE NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya mwisho imethibitisha kuwa angalau watu 28 wameuawa, mamia wengine wamejeruhiwa. Shambulio hilo limelenga kundi la vijana ambao walikuwa wakijiandaa kujielekeza katika mji wa Kikurdi wa Kobani nchini Syria ambapo shambulio jingine limetokea wakati huo huo. Kwa mujibu wa naibu mkuu wa Suruç, " inawezekana huenda shambulio hilo limetekelezwa na kundi la Islamic State."

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Istanbul, Jérôme Bastion, vijana zaidi ya 300 wa kujitolea, waliokusanyika chini ya chini ya mwamvuli wa Shirikisho la vijana wa Kisoshalisti, walikua wamewasili kutoka mji wa Istanbul kwa basi na walikuwa wakijianda kuelekea katika mji wa Kikurdi wa Kobanî, nchini Syria, kwa lengo la kushiriki katika ujenzi wa mji huo.

Wakati wa mlipuko, walikuwa wamekaa kwa ajili ya kifungua kinywa kiliongozana na mkutano wa waandishi wa habari katika bustani ya Kituo cha Utamaduni wa mji wa Suruç, karibu na mpaka wa Syria.

Shambulio katika mji wa Kobanî

Muda mfupi baada ya mlipuko wa Suruç, shambulio jingine la bomu lililotegwa katika gari limetokea pia katika mji wa Kobanî, karibu kilomita 5 na upande wa Syria. Kwa mujibu wa Rami Abdel Rahman, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali nchini Syria, "mshambuliaji wa kujitoa mhanga amelipua bomu lililokua limetegwa katika gari katika eneo la ukaguzi kusini mwa Kobanî. Wapiganaji wawili wa Kikurdi wameuawa kwa mlipuko huo."

Katika mji wa Suruç, watu wengi wanahusisha kundi la Islamic State kwa shambulio hilo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, ambalo limenukuu chanzo rasmi cha Uturuki, viongozi wa Uturuki wana " Sababu za msingi " kuamini kwamba Islamic State ndio imehusika na shambulio hilo.

Kama taarifa hii ingelithibitishwa, itakuwa mara ya kwanza kundi la Islamic State kuendesha mashambulizi katika ardhi ya Uturuki tangu kundi hili lilipoundwa. Islamic State imeendelea kudhibiti baadhi ya maeneo nchini Iraq na Syria, hususan karibu na Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.