Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Mashambulizi: Ufaransa yahamasisha washirika wake

Kuna gari ambayo imepatikana katika mji wa Paris, ambayo inakisiwa kuwa ilitumiwa na watu walioendesha mashambulizi usiku wa Ijumaa iliopita, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya zaidi ya watu 129 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 350.

Rais Hollande na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika Ikulu ya Elysée, Novemba 17, 2015.
Rais Hollande na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry katika Ikulu ya Elysée, Novemba 17, 2015. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wachunguzi wamekuwa wakijaribu Jumanne hii kuchunguza njia walizotumia wahusika wa mashambulizi ya jijini Paris, ambapo mmoja miongoni mwa watuhumiwa yuko mafichoni.

Ufaransa imeendelea na harakati zake za kuhamasisha washirika wake dhidi ya kundi la Islamic State (EI) ncini Syria.

François Hollande atakutana na Rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington Novemba 24 na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow Novemba 26, katika matumaini ya kufikia muungano wa kipekee kwa "kulitokomeza" kundi la Islamic State. Rais wa Urusi ameagiza majeshi yake ya majini "kushirikiana" na Ufaransa.

Rais Hollande tayari amekutana Jumanne wiki ii katika Ikulu ya Elysée na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry. Kiongozi huyo wa Marekani amesema kuwa Syria ilikuwa labda katika "wiki" wachache tu ili ipate taasisi za mpito ambapo serikali ya Damascus na upinzani vingegawana.

Paris pia imeomba msaada wa kijeshi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya (EU), baada ya mashambulizi ya ndege za jeshi la Ufaransa katika mkoa wa Raqa, ngome ya kundi la Islamic State, kaskazini mwa Syria.

Watu wawili waliokamatwa Jumamosi katika wilaya ya Molenbeek katika eneo maarufu jijini Brussels, kitovu cha wanajihadi, walioshtakiwa na Ofisi ya mashtaka ya Ubelgiji kwa kosa la "Ugaidi" wanashukiwa kuwa walishiriki katika mashambulizi hayo ya Paris. Wawili hao ni Mohammed Amri, mwenye umri wa miaka 27, na Hamza Attou, mwenye umri wa miaka 20.

Mfaransa akiri kuhuska katika mauaji yaliotokea Paris Novemba 13

Wanajihadi wengine, ambao ni Wafaransa, ambao wanafuatiliwa kwa karibu na wachunguzi ni Fabien Clain, mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa mkoa wa Toulouse, mwenye msimamo mkali, ni mtu ambaye alisikika katika sauti iliorekodiwa akikiri kuhusika kwa niaba ya Kundi la Islami State mashambulizi yalitokea usiku wa Ijumaa Novemba 13 jijini Paris, vyanzo vilio karibu na uchunguzi vimeliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.