Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Abaaoud, mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris, afariki

Abdelhamid Abaaoud amefariki. Mwili wa mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris umetambuliwa Alhamisi hii na wachunguzi baada ya polisi kuendesha operesheni Jumatano wiki hii dhidi ya ghorofa katika kitongoji kimoja kaskazini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Abdelhamid Abaaoud, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco.
Abdelhamid Abaaoud, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco. capture d'écran youtube
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Manuel Valls amekaribisha ujasiri wa polisi kwa kumuangamiza "muhusika mkuu" wa mashambulizi, na kuacha wazi uwezekano wa kutokomeza kundi la wahusika wengine wa mashambulizi yaliogharimu maisha ya zaidi ya watu 129 na kuwajeruhiwa wengine352.

Jumatano asubuhi baada ya milio ya risasi kusikika, polisi lilivamia ghorofa moja katika eneo la Saint-Denis (Seine-Saint-Denis) kufuatia ushahidi ulioonyesha kuwa Abdelhamid Abaaoud alikuwa nchini Ufaransa.

Mwili wake "umetambuliwa rasmi", "baada ya kufananisha" alama za vidole, mwendesha mashtaka, François Molins, amebaini. "Hata hivyo, haijafahamika iwapo Abaaoud alijilipua au la ", Ofisi ya mashitaka imesema.

Akijulikana kwa jina la utani la Abu Omar al-Baljiki ("Ubelgiji" kwa Kiarabu), Mbeleji huyo mwenye asili ya Morocco, mwenye umri wa miaka 28 , ambaye amekua akitafutwa ni mmoja wa wanajihadi wa kundi la Islamic State wanaozungumza Kifaransa. Kundi la Islamic State (IS) lilikiri mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa lilihusika katika mashambulizi ya Novemba 13 jijini Paris.

"Mashambulizi sita yalishindwa au yalitibuliwa na vyombo vya usalama vya Ufaransa tangu majira ya joto mwaka 2015, Abaaoud alihusika katika amshambulizi 4 kati hayo", Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve amesema.

Ulaya "inapaswa kufanya kila kilio cini ya uwezo wake ili kushinda ugaidi", Cazeneuve ameongeza siku moja kabla ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya ndani jijini Brussels.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.