Pata taarifa kuu
UHAMIAJI-DENMARK

Wahamiaji: Denmark yapitisha marekebisho yenye utata kuhusu haki ya ukimbizi

Bunge la Denmark limepitisha Jumanne hii mageuzi yenye utata kuhusu sheria ya uhamiaji ambayo ina lengo la kukatisha tamaa waombaji hifadhi wanaojaribu bahati zao katika nchi za Scandinavia, kufuatia mikataba ya kimataifa.

Waziri Mkuu wa zamani wa Denmark Helle Thorning Schmidt (kushoto) na Waziri wa Uhamiaji Inger Stojberg (kulia) Katika Bunge wakati wa mjadala juu ya mageuzi kuhusu uhamiaji, Januari 25, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani wa Denmark Helle Thorning Schmidt (kushoto) na Waziri wa Uhamiaji Inger Stojberg (kulia) Katika Bunge wakati wa mjadala juu ya mageuzi kuhusu uhamiaji, Januari 25, 2015. REUTERS/Marie Hald/Scanpix Denmark
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Lars Løkke Rasmussen, ambaye serikali yake inayoungwa mkono na watu kutoka chama maarufu nchini Dernmark wanaopinga suala la uhamiaji, amekubali kikamilifu uidhinishwaji wa kile alichokiita "Muswada wa sheria ulioeleweka vibaya katika historia ya Denmark" .

Akikemewa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya maendeleo na uchumi barani Ulaya na mashirika ya kibinadamu, Rasmussen ameendelea kushikilia msimamo, baada ya kungwa mkono na raia wake: kulingana na utafiti uliofanywa, 70% ya raia wa Denmark wanatiwa wasiwasi na uhamiaji.

"Wakimbizi wengi wanavuka mipaka yetu, tunakabiliwa na shinikizo kubwa", amesema Waziri wa Uhamiaji, Ushirikiano na Makazi, Inger Støjberg, huku akisubiriwa mjini Brussels na Kamati ya Bunge inayoshugulikia masuala ya uhuru wa raia.

Shirika la Umoja wa Mataiafa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) linaushtumu muswada huo wa sheria kwamba unakuza "hofu na ubaguzi kwa wageni". Muswada huo wa sheria ambao unatazamiwa kuidhinishwa Jumanne hii unapania kupokonya haki za wahamiaji, kupunguza haki zao za kijamii, na kurefusha muda wa kuungana kwa familia na kupewa kibali cha kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.