Pata taarifa kuu
UBELGIJI-AJIRA

Maandamano makubwa dhidi ya "sheria ya kazi" Ubelgiji

Wafanya fujo, waliofukuzwa na polisi kwa kutumia mizinga ya maji, wamevuruga maandamano makubwa mapya yaliyokua yamefikia ukingoni nchini Ubelgiji dhidi ya mageuzi, hasa ya sheria ya kazi, yanayopangwa kufanywa na serikali ya mrengo wa kulia.

Watu 60,000 wamekusanyika katika mji wa Brussels wakipinga dhidi ya marekebisho ya sheria ya kazi Ubelgiji.
Watu 60,000 wamekusanyika katika mji wa Brussels wakipinga dhidi ya marekebisho ya sheria ya kazi Ubelgiji. @ ERIC LALMAND / Belga / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya watu wapatao 60,000, kwa mujibu wa polisi, yamevunjwa karibu na eneo la Gare du Midi mjini Brussels ambapo mamia ya wafanya fujo, baadhi wakiwa wamejificha nyuso zao kwa fulana au vifaa vya kujilinda na gesi, walianza kutupa vilipuzi dhidi ya polisi, ambayo ilijibu kwa mizinga ya maji.

Waandamanaji wanane na askari polisi wawili, ikiwa ni pamoja afisa mmoja, wamejeruhiwa, kwa mujibu wa polisi, iliyonukuliwa na shirika la habri la Belga.

Maandamano, ambayo yaliitishwa na vyama vya vikuu vya wafanyakazi nchini Ubelgiji lakini pia chama cha Kisoshalisti (PS) ambacho kiko katika kambi ya upinzani tangu uchaguzi wa mwaka 2014, tangu wakati huo yalikua yakiendeshwa kwa utulivu, waandamanaji wakizunguka maeneo makuu ya katikati ya mji mkuu wa Ubelgiji katika hali ya utulivu na amani.

Katika msafara wa maandamano hayo, waandamanaji kutoka mikoa ya Flanders (kaskazini), Wallonia (kusini) na Brussels walikua wamebeba mabango ambayo yalikua yameandikwa kama vile "hapana kwa wiki ya masaa 45", "isiguswi pensheni yetu" au pia "Hapana mabadiliko " na walikuwa wakilipua maputo mengi.

Mwaka mmoja na nusu baada ya kuingia madarakani muungano wa mrengo wa kulia wa Waziri Mkuu Charles Michel, uhamasishaji wa vyama vya wafanyakazi na vyama vya kisiasa vya mrengo wa kushoto kumeendelea kuwa na nguvu. Migomo kadhaa ilishuhudiwa mwaka 2014 baada ya maandamano makubwa katika mji wa Brusselsmwezi Novemba 2014, ambapo watu 120,000 walishiriki, kamwe tukio hilo lilikua halijaonekana kwa miongo kadhaa nchini Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.