Mkutano wa Baraza la Ulaya waahirishwa hadi Oktoba 1 na 2, Charles Michel ajiweka karantini
Mkutano wa Baraza la Ulaya, uliokuwa umepangwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa, umeahirishwa hadi 1 na 2 Oktoba, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, amejiweka kizuizini baada ya kutangamana wiki iliyopita na mtu aliye ambukizwa virusi vy Corona, msemaji wake amesema.
Imechapishwa:
Charles Michel hakupatikana na ugonjwa huo baada ya kufanya vipimo siku ya Jumatatu lakini anafuata sheria za kujiweka karantini zinazotumika nchini Ubelgiji, amesema msemaji wake.
Kufikia sasa ugonjwa wa COVID-19 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 966,000. Watu Milioni 31,4 wameambukizwa virusi vya Corona na Milioni 21,5 wamepona ugonjwa huo hatari.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.