Wajerumani wajiandaa kupiga kura siku ya Jumapili
Kampeni za mwisho zinafanyika kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini Ujerumani siku ya Jumapili, utakaomaliza uongozi wa miaka 16 wa Kansela Angela Merkel.
Imechapishwa:
Wapiga kura wapatao Milioni 60 walio na zaidi ya umri wa miaka 18 wanatarajiwa kushiriki kwenye Uchaguzi huo, kuwachagua wabunge 598.
Wachambuzi wa siasa wanasema, utachaguzi huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kati ya chama cha Kansela Merkel cha CDU na kile cha mrengo wa Kushoro cha SPD.
Tayari Merkel ameunga mkono kiongozi wa chama chake Armin Laschet kumrithi, anapomaliza muda wake wa uongozi nchini humo.
Katika kampeni ya mwisho siku ya Jumamosi, Kansela Merkel amempigia debe Laschet na kuwataka Wajerumani kumchagua wakati huu kura za maoni zikionesha kuwa yupo nyuma ya mgombea wa SPD Olaf Scholz.