Pata taarifa kuu
UINGEREZA-HAKI

Mahakama ya Uingereza yataka Julian Assange akabidhiwe Marekani

Mahakama Kuu ya London imebatilisha hukumu ya mahakama ya mwanzo ya kukataa kumkabidhi mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange, kwa Marekani. Washington inataka kumhukumu kwa uvujaji mkubwa wa nyaraka.

Maandamano ya kumuunga mkono Julian Assange. Katika uamuzi wake Ijumaa hii, Mahakama inazingatia kwamba Washington imetoa hakikisho juu ya usalama wa mwanzilishi wa WikiLeaks kama atarejeshwa Marekani.
Maandamano ya kumuunga mkono Julian Assange. Katika uamuzi wake Ijumaa hii, Mahakama inazingatia kwamba Washington imetoa hakikisho juu ya usalama wa mwanzilishi wa WikiLeaks kama atarejeshwa Marekani. JOHN THYS AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Uingereza "inaidhinisha rufaa" iliyoletwa na Marekani, amesema Jaji Tim Holroyde, ambayo ina maana kwamba uamuzi wa mahakama ya mwanzo umefutwa na kwamba mahakama italazimika kutoa uamuzi tena juu ya ombi la kurejeshwa kwa Marekani. Takriban mwaka mmoja uliopita, Jaji Vanessa Baraitser alipinga kukabidhiwa kwa raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 50 kwa mamlaka ya Marekani, akitaja hatari ya kujiua kwa mwanzilishi wa WikiLeaks.

Katika uamuzi wake Ijumaa hii, Mahakama Kuu inazingatia kwamba Marekani imetoa hakikisho juu ya usalama wa mwanzilishi wa WikiLeaks ikiwa atarejeshwa, hivyo kujibu wasiwasi wa jaji wa mahakama. Mpenzi na wakili wa Julian Assange, Stella Moris, amelaani kile aichokitaja kama "kosa kubwa wa kimahakama", katika taarifa iliyotumwa na WikiLeaks.

Hati za siri 700,000

Marekani inamtuhumu Julian Assange kwa kuchapisha zaidi ya nyaraka 700,000 zilizoainishwa kuhusu shughuli za kijeshi na kidiplomasia za Marekani, hasa nchini Iraq na Afghanistan, kuanzia mwaka wa 2010. Akiwa amefunguliwa mashitaka hasa ya ujasusi, Julian Assange anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 175 jela katika kesi ambayo, kulingana na wafuasi wake, inaonesha shambulio baya sana dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International limejibu kwa sauti ya mkurugenzi wake barani Ulaya akishutumu kile alichosema ni "makosa ya kimahakama". "Iwapo atarejeshwa Marekani, Julian Assange hataweza tu kuhukumiwa chini ya Sheria ya Ujasusi lakini pia itahatarisha ukiukwaji mkubwa wa haki zake za kibinadamu kutokana na masharti yake ya kizuizini ambayo yanaweza kuhusisha mateso au unyanyasaji mwingine," Nils Muižnieks. amesema katika taarifa.

Akiwa amefungwa katika gereza lenye ulinzi mkali karibu na London, Julian Assange alikamatwa na polisi wa Uingereza mmwezi Aprili 2019 baada ya kukaa miaka saba katika Ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza ambako alikuwa amekimbilia wakati alikuwa aliachiliwa huru kwa dhamana. Alihofia kurejeshwa nchini Marekani au Sweden, ambako alishtakiwa kwa ubakaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.