Meli mbili za mizigo zagongana kusini mwa Sweden, watu kadhaa watoweka
Meli mbili za mizigo ziligongana mapema usiku, Jumatatu asubuhi, Desemba 13, kusini mwa Sweden, na kusababisha kupinduka kwa meli moja na mabaharia wawili kuzama baharini, kulingana na mamlaka ya baharini ya Sweden.
Imechapishwa:
Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa 2:30 saa za kimataifa, katika Bahari ya Baltic kati ya ncha ya kusini ya Sweden na kisiwa cha Denmark cha Bornholm kati ya meli ya mizigo ya Uingereza na meli ya Denmark, ambayo ndiyo iliyopinduka, msemaji wa mamlaka hiyo, Carl- Johan Linde ameliambia shirika la habari la AFP.
Watu kadhaa wanahofiwa kuwa majini na operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, shirika la utangazaji la umma la Uswidi SVT liliripoti Jumatatu
Operesheni kubwa ya uokoaji inayohusisha boti tisa na helikopta inaendelea, katika maji baridi sana, yenye digrii nne tu.