Pata taarifa kuu

Ukraine yakusanya wanajeshi wake wa akiba na kutoa wito kwa raia wake kuondoka Urusi

Ukraine imezindua zoezi la kuhamasisha askari wa akiba wa jeshi lake na kuwataka raia wake kuondoka Urusi haraka iwezekanavyo kwa sababu ya hofu ya kuongezeka mzozo kati ya nchi hizo mbili. Hata hivyo, Baraza la Usalama la Ukraine limetoa wito wa kutangazwa kwa hali ya hatari.

Askari wa akiba wanashiriki katika mafunzo huko Kiev mnamo Februari 19, 2022.
Askari wa akiba wanashiriki katika mafunzo huko Kiev mnamo Februari 19, 2022. REUTERS - ANTONIO BRONIC
Matangazo ya kibiashara

"Uhamasishaji unaanza leo. Muda wa juu wa huduma hiyo ni mwaka mmoja," vikosi vya ardhini vya Ukraine vimetangaza kwenye ukurasa wao wa Facebook. Tangazo ambalo linakuja baada ya uamuzi wa Vladimir Putin wa kutambua uhuru wa maeneo yaliyojitenga mashariki mwa Ukraine. Nchi hiyo ina askari wa akiba zaidi ya 200,000 pamoja na wanajeshi 250,000 wa vikosi vya kawaida vya jeshi.

"Uhamasishaji huo utahusu askari wa akiba wenye umri wa miaka 18 hadi 60", pia imebainishwa. Kukataa kuonekana kwa zoezi la kujiandikisha bila sababu inayoeleweka kunaweza kuwa chini ya "vikwazo vya kiutawala na jinai", vikosi vya jeshi vimebaini.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky hata hivyo alifutilia mbali siku moja kabla katika hotuba yake ya televisheni "uhamasishaji wa jumla" huku wabunge wa Urusi wakiruhusu Kremlin kupeleka jeshi lake katika maeneo ya Ukraine yaliyojitenga.

Waukraine milioni tatu nchini Urusi

Kiev pia imetoa wito kwa raia wake siku ya Jumatano kuondoka Urusi haraka iwezekanavyo, katika hali ya "kuongezeka kwa vitisho vya Urusi dhidi ya Ukraine", inaeleza taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje. Karibu watu milioni tatu wa Ukraine wanaishi Urusi, kulingana na mamalaka nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.