Pata taarifa kuu

Biden alaani 'shambulio lisilo la msingi' la Urusi dhidi ya Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden ameshutumu "shambulio lisilo la msingi" la Urusi dhidi ya Ukraine Jumatano jioni, baada ya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kutangaza "operesheni ya kijeshi" kuwatetea wanaotaka kujitenga mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Marekani Joe Biden amekosoa 'shambulio lisilo la msingi' la Urusi dhidi ya Ukraine.
Rais wa Marekani Joe Biden amekosoa 'shambulio lisilo la msingi' la Urusi dhidi ya Ukraine. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

"Rais Putin amechagua (kuanzisha) vita vilivyokusudiwa ambavyo vitasababisha mateso na hasara kubwa ya binadamu," Biden alisema katika taarifa yake. "Urusi pekee ndiyo inahusika na vifo na uharibifu utakaosababishwa na mashambulizi haya," alisisitiza.

Vladimir Putin atangaza "operesheni ya kijeshi" nchini Ukraine

Viongozi kadhaa wa Marekani waliochaguliwa katika pande zote mbili wamekosoa uamuzi wa Bw. Putin.

Seneta wa chama cha Democratic Mark Warner, mkuu wa Kamati ya Ujasusi, amehimiza Marekani na NATO "kuungana" kukabiliana na majaribio ya "Putin kutaka kuanzisha ufalme wa Urusi kwa gharama ya watu wa Ukraine".

"Kwa zaidi ya miaka 70 tumeepuka vita kamili barani Ulaya. Kwa uvamizi wake haramu nchini Ukraine, Vladimir Putin amemaliza miongo ya amani kwa jumla," ameandika.

Seneta wa chama cha Republican Mitt Romney alitoa wito kwa Marekani na washirika wake "kulinda uhuru" kwa kuweka "Putin na Urusi katika vikwazo vikali zaidi vya kiuchumi, kuwafukuza kutoka kwa taasisi za kimataifa na kujitolea katika upanuzi na kisasa kw ulinzi wa taifa letu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.