Pata taarifa kuu

Ukraine yadai kuwa mauaji ya raia Boutcha yalikuwa 'ya makusudi'

Katika siku ya 39 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumapili hii Aprili 3, wakati Ukraine ikitangaza kuwa imelikomboa kabisa eneo la kyiv, milio ya mizinga imechukuwa na fasi ya kutoa heshima kwa maiti za raia zilizozagaa mitaani katika baadhi ya miji iliyoharibiwa.

Charles Michel ameshutumu "ukatili" uliofanywa na jeshi la Urusi, katika maeneo kama Boutcha.
Charles Michel ameshutumu "ukatili" uliofanywa na jeshi la Urusi, katika maeneo kama Boutcha. AFP - RONALDO SCHEMIDT
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Mashambulizi mbalimbali yamelenga miundombinu katika bandari ya Odessa Jumapili asubuhi.

► Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi karibu na Kyiv, Waukraine wamerudi katika miji yao iliyoharibiwa kwa kiasi na maiti nyingi za raia zikiwa zimetapakaa mitaani, kama huko Boutcha. Baadhi ya watu walikuwa wamefungwa mikono walipouawa. Charles Michel, mkuu wa Umoja wa Ulaya ameshutumu "ukatili" na kutoa wito wa vikwazo vipya.

► Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa Jumapili hii huko Moscow ambapo atajaribu kupata hakikisho la "usitishwaji mapigano" nchini Ukraine.

► Mpatanishi mkuu wa Urusi siku ya Jumapili alighadhabishwa na matamshi ya mwenzake wa Ukraine ambaye alikuwa amebaini Jumamosi jioni kwamba Moscow ilikuwa imekubali "kwa maneno" mapendekezo makuu ya Ukraine.

Moscow imeondoa vikosi vyake vingi katika siku za hivi karibuni katika mikoa ya Kyiv na Chernigiv, kaskazini mwa Ukraine, na kutangaza kwamba inataka inawekeza nguvu zaidi katika mkoa wa mashariki wa Donbass, pamoja na jiji lililozingirwa la Mariupol.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.