Pata taarifa kuu

Urusi yasema iko tayari kwa makubaliano ya kusitisha vita katika eneo la Azovstal

Katika siku ya 58 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hatima ya bandari ya kimkakati ya Mariupol, ambayo Moscow inadai kuwa "imekomboa", bado haijulikani. Kyiv inasema watu wake bado wanapigana na vikosi vya Urusi katika kiwanda kikubwa cha madini katika eneo la Azovstal huko Mariupol.

Picha ya setilaiti iliyopigwa Aprili 20, 2022 juu ya kiwanda cha chuma cha Azovstal, ambapo wanajeshi wa Ukraine bado wanapigana.
Picha ya setilaiti iliyopigwa Aprili 20, 2022 juu ya kiwanda cha chuma cha Azovstal, ambapo wanajeshi wa Ukraine bado wanapigana. AP
Matangazo ya kibiashara

"Moja ya malengo ya jeshi la Urusi ni kuweka udhibiti kamili katika mji wa Donbass na kusini mwa Ukraine", afisa mkuu wa jeshi la Urusi alisema Ijumaa, akizungumzia "awamu ya pili ya operesheni maalum" inayolenga, pamoja na mambo mengine, " kuhakikisha kumekuwa na eneosalama la kiutu kuelekea Crimea."

Bandari ya kimkakati ya Mariupol, ambayo Moscow inadai "imekomboa", bado wanajeshi wa Ukraine wanapigana na vikosi vya Urusi, inasema Kyiv, ambayo inabaini kwamba wapiganaji wa wa Ukraine wanaendelea kutetea vikali kiwanda kikubwa cha chuma huko Azovstal, ambapo raia pia wamekimbilia.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amemwomba Rais wa Urusi Vladimir Putin leo Ijumaa ahakikishe kuna kuwa na maeneo ya usalama wa kiutu huko Mariupol wakati wa Pasaka ya Kiorthodoksi. Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alitangaza kuwa hakuna maeneo ya usalama wa kiutu yatakayowekwa Ijumaa hii, hali ikiwa ni "hatari" sana barabarani.

Umoja wa Mataifa umeshutumu jeshi la Urusi kwa vitendo ambavyo "vinaweza kuwa uhalifu wa kivita" nchini Ukraine. Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wameandika "mauaji, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela" ya raia 50 katika mji wa Bucha, nje kidogo ya mji wa Kyiv, ambapo vikosi vya Urusi vinashutumiwa kufanya mauaji yaliosababisha vifo vya makumi ya watu. Madai ambayo Moscow inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.