Pata taarifa kuu
WHO- AFYA

EU imeidhinisha chanjo ya ndui kutumika dhidi ya monkeypox

Umoja wa ulaya umeidhinisha chanjo ya ndui kutumika dhidi ya ugonjwa wa monkeypox hatua inayokuja baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza maambukizi hayo kama janaga la kiafya imedhibitisha kampuni yakutengeneza dawa ya nchini Denmark iliyotengeneza chanjo hiyo.

Chanjo ya monkeypox
Chanjo ya monkeypox REUTERS - DADO RUVIC
Matangazo ya kibiashara

WHO katika taarifa yake ya siku ya Jumamosi, ilidhibitisha kuwa watu 16,000 wameambukizwa katika mataifa 75 duniani ikitaka mataifa ya dunia kuchukulia swala hili kwa umakini.

Imvanex imekuwa ikitumika katika mataifa ya bara ulaya tangu mwaka wa 2013 kuzuia maambukizi ya ndui.

Hatua ya kuidhinishwa kwa chanjo hiyo imeafikiwa kutokana na hali kuwa virusi vinavyosababisha monkeypox vinafana na vile vinavyosababisha ndui.

Imefahamika kuwa Monkeypox sio hatari kama ndui maambukizi yaliomalizika mwaka wa 1980.

Dalili za kwanza za monkeypox ni joto, kuumwa na kichwa, misuli na magongo katika kipindi cha siku tano za maambukizi hayo.

Maambukizi ya monkeypox yameripotiwa tangu mapema mwezi Mei nje ya mataifa ya Afrika magharibi na kati maeneo ambayo yamekuwa yakiripoti ugonjwa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.