Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Denmark inataka kuongeza mara tatu matumizi yake ya kijeshi ndani ya miaka 10

Denmark imetangaza Jumanne Mei 30 kwamba itaongeza mara tatu matumizi yake ya kijeshi katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Uwekezaji wa taji za Denmark bilioni 143 (sawa na euro bilioni 19.2) kufikia 2% ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2030, hitaji la NATO.

Wanajeshi wa jeshi la Denmark wakiwa katika mazoezi huko Oksboel, magharibi mwa Denmark, Machi 16, 2023.
Wanajeshi wa jeshi la Denmark wakiwa katika mazoezi huko Oksboel, magharibi mwa Denmark, Machi 16, 2023. © Mads Claus Rasmussen / AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Carlotta Morteo

Je, takwimu za bajeti ya ulinzi zitakidhi mahitaji? Hifadhi za risasi na vifaa vingine vya kijeshi ni tupu, meli ambazo zimezeeka, ndege chache mno. Tangu 2017, matumizi ya kijeshi ya Denmark yameongezeka polepole, bila shaka, lakini yalikuwa yamefikia kiwango cha chini cha kihistoria, cha 1.14% tu ya Pato la Taifa.

Vita vya Ukraine vimechochea hitaji la Denmark kuimarisha majeshi haya, kurekebisha vifaa vyake vya kisasa na kuanzisha mpango wa miaka 10 ijayo. Na hakika ni alama ya mataji haya bilioni 143 yaliyotangazwa ambayo sasa yatakuwa mada ya mijadala mikali.

Bajeti ikiwa ni pamoja na misaada kwa Ukraine

Mambo mawili yako wazi: Urusi ndio tishio kuu, na usalama wa Denmark unategemea usalama wa kikanda na vipaumbele vikuu vitatu. Kwa Denmark, ni muhimu kupata Bahari ya Baltic, kufuatilia vyema ukanda wa urambazaji wa kilomita 2,900 ambao unatoka Copenhagen hadi Greenland, na ambapo meli za Urusi kaskazini zinapita ili kufikia bahari Atlantiki, na hatimaye kuhakikisha usalama wa ghala za Denmark , ikiwa ni muhimu kwa vikosi vyote vya NATO.

Ikumbukwe kwamba bajeti ya Ulinzi hutoa taji bilioni 21 za msaada wa kijeshi kwa Kyiv, pesa ambazo zinaongezwa kwa Mfuko Maalum na pia kwa vifurushi mbalimbali vya misaada vilivyotangazwa tayari. Denmark ikiwa imeahidi Ukraine kuiunga mkono kwa muda mrefu iwezekanavyo, kwa sababu ushindi wake unaonekana kama sababu ya wazi ya utulivu wa kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.