Pata taarifa kuu

AC Milan yampongeza Berlusconi, rais wake wa zamani 'asiyesahaulika'

Ikizshikiliwa na Silvio Berlusconi kwa zaidi ya miaka thelathini, kati ya mwaka 1986 na 2017, AC Milan imesema kufuatia kifo cha rais wake wa zamani. "AC Milan, kwa huzuni kubwa, inaomboleza kifo cha Silvio Berlusconi asiyesahaulika," imesema klabu hiyo.

Kiongozi wa chama cha Forza Italia Silvio Berlusconi katika Seneti, mjini Rome, Oktoba 26, 2022. Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi alilazwa hospitalini Jumatano, Aprili 5, 2023, akiwa na matatizo ya kupumua, vyombo vya habari vya Italia viliripoti. Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 86 alikuwa katika uangalizi mahututi katika hospitali ya Milanâs San Raffaele, ambayo hupokea huduma mara kwa mara, shirika la habari la LaPresse, Sky TG24 na Corriere della Sera liliripoti, bila kutaja vyanzo.
Kiongozi wa chama cha Forza Italia Silvio Berlusconi katika Seneti, mjini Rome, Oktoba 26, 2022. Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi alilazwa hospitalini Jumatano, Aprili 5, 2023, akiwa na matatizo ya kupumua, vyombo vya habari vya Italia viliripoti. Waziri Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 86 alikuwa katika uangalizi mahututi katika hospitali ya Milanâs San Raffaele, ambayo hupokea huduma mara kwa mara, shirika la habari la LaPresse, Sky TG24 na Corriere della Sera liliripoti, bila kutaja vyanzo. AP - Andrew Medichini
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya rossonero - nyekundu na nyeusi - ilichukuliwa kuwa kumbukumbu ya kandanda ya Ulaya wakati mkuu wa zamani wa serikali ya Italia alipokuwa rais wake, katika ujumbe kwenye tovuti yake. "Asante rais, milele pamoja nasi," Ac Milan imeongeza.

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti Jumatatu ametoa "shukrani zake nyingi" kwa Silvio Berlusconi, ambaye "alifanya maamuzi" katika maisha yake kama nahodha na kocha katika AC Milan. "Huzuni ya leo haifuti nyakati za furaha tulizozitumia pamoja", ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter mchezaji huyo wa zamani kuanzia mwaka 1987 hadi 1992 na kocha wa klabu ya AC Milan kuanzia mwaka 2001 hadi 2009. AC Monza, ambayo alichukua mwaka wa 2018, mwaka mmoja baada ya kuiuza Milan, na Adriano Galiani, mhirika wa karibu wa muda mrefu wa Silvio Berlusconi, pia alitoa heshima kwa mkuu wa zamani wa serikali ya Italia.

Vladimir Putin anatoa pongezi kwa "rafiki wa kweli"

Nchini Ufaransa na kimataifa, rambi rambi zulikuja haraka kutoka kwa mrengo wakulia na wakushoto. "Kiongozi asiye wa kawaida, mwenye maisha ya ajabu na kazi ya kupendeza, Silvio Berlusconi aliashiria maisha ya kisiasa ya Italia bila shaka. Kwa Italia iliyo katika maombolezo, ninatuma salamu zangu za rambirambi, "ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Marine Le Pen. "Ukumbusho wa kweli wa siasa nchini Italia na kiongozi ambaye alihudumu kwa nguvu zake zote, alikuwa mtetezi wa dhati wa urafiki kati ya mataifa yetu mawili. Ninatuma rambirambi zangu kwa ndugu zake na raia wa Italia, "amesema kiongozi wa chama cha Republican, Eric Ciotti.

Kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, akizungumza kupitia msemaji wake rasmi, "Silvio Berlusconi ameacha alama kubwa katika siasa za Italia kwa miongo kadhaa". Kwa upande wake, Viktor Orban amepongeza ujasiri wa "mpiganaji mkuu".

Rais wa Urusi Valdimir Putin pia ametoa pongezi kwa Silvio Berlusconi. "Kwangu mimi, Silvio alikuwa mtu mpendwa, rafiki wa kweli," amesema, katika telegramu ya rambirambi iliyoelekezwa kwa Rais wa Italia Sergio Mattarella. Rais wa Urusi amesema kila mara alivutiwa na "hekima" yake na kusifu "nguvu yake ya ajabu", "matumaini" yake na "ucheshi" wake, kulingana na taarifa kutoka Kremlin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.