Pata taarifa kuu

Ukraine yaishutumu Hungary kwa kuzuia upatikanaji wa wafungwa wake wa kivita

Je, Budapest inazuia Kyiv kupata kundi la wafungwa wa kivita wa Ukraine waliohamishiwa Hungary? Kwa vyovyote vile, hivi ndivyo msemaji wa diplomasia ya Ukraine anasema, akishutumu mamlaka ya Hungary kwa kukiuka Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu, madai ambayo Budapest inakanusha, ikidai kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria na sheria zinazotumika kimataifa.

Mwanajeshi wa Ukraine akibadilisha ngome yake kukabiliana na wanajeshi wa Urusi karibu na Bakhmut, eneo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Mei 2, 2023.
Mwanajeshi wa Ukraine akibadilisha ngome yake kukabiliana na wanajeshi wa Urusi karibu na Bakhmut, eneo la Donetsk, Ukraine, Jumanne, Mei 2, 2023. AP - Libkos
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Juni 8, Kanisa la Othodoksi la Urusi liliingilia kati, na bila mamlaka ya Ukraine kufahamishwa, Waukraine 11, wafungwa wa kivita kulingana na Kiev, walihamishiwa Hungary kutoka Urusi. Raia wa Ukraine kutoka Transcarpathia, eneo lililo magharibi mwa Ukraine lenye jamii kubwa ya Wahungary.

Tangu wakati huo, "majaribio yote ya wanadiplomasia wa Ukraine kuanzisha mawasiliano ya moja kwa moja na raia hao yalionekana kutofaulu," anaeleza msemaji wa diplomasia ya Ukraine, ambaye anaishutumu Budapest kwa kuwaweka kando, bila njia yoyote ya mawasiliano. Vitendo hivi vya kulaaniwa vinatetewa na mamlaka ya Hungary, ambayo inaeleza kwamba Waukraine hao hawachukuliwi kama wafungwa wa kivita katika ngazi ya kisheria tangu walipoachiliwa katika ardhi ya Urusi.

"Wako hapa kwa hiari yao wenyewe, wanaweza kuondoka nchini kwa uhuru wakati wowote, hatuhusiki nao wala hawafuatiliwi na vyombo vyetu vya sheria," anaelezea mkurugenzi wa ofisi ya Waziri Mkuu Viktor Orban. Lakini Kiev haikubaliani na hoja hiyo na kwa mara nyingine tena inatoa wito kwa serikali ya Hungary kumpa balozi wa Ukraine nafasi ya kukutana haraka na wafungwa hawa wa kivita "ili aweze kutathmini hali yao ya kiakili na kisaikolojia, kuwaelezea haki zao na kutoa msaada wa dharura wa kibalozi".

Sehemu moja zaidi katika uhusiano wwenye mvutano kati ya nchi hizi mbili tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi, ikijulikana kuwa Hungary ndio nchi pekee ya Ulaya inayoendeleza ushirikiano na mawasiliano na Moscow.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.