Pata taarifa kuu

Uhispania: Watatu wafariki na watatu hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha

Baada ya miezi kadhaa ya ukame wa kihistoria, Uhispania inakumbwa na mvua kubwa iliyosababisha vifo vya watu watatu na watatu hawajulikani waliko, huku mtoto wa miaka kumi akinusurika kuzama baada ya kukimbilia kwenye mti.

Mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Madrid, Septemba 4, 2023.
Mvua kubwa iliyonyesha katika jimbo la Madrid, Septemba 4, 2023. AFP - OSCAR DEL POZO CANAS
Matangazo ya kibiashara

Mvua hizi, ambazo zimekuwa zikiathiri nchi tangu mwishoni mwa wiki hii, zimeathiri hasa mikoa ya Madrid na Castile-La Mancha, katikati mwa Uhispani, ambako mvua ilinyesha usiku wa siku ya Jumapili kuamkia Jumatatu.

Rais wa Castile-La Mancha, Emiliano García-Page, alitangaza Jumatatu asubuhi kwenye mitandao ya kijamii "vifo vya watu wawili katika jimbo la Toledo", katika maeneo ya Casarrubios del Monte na Bargas. Hakutoa maelezo kuhusiana na mazingira ya vifo hivyo.

Walinzi wa Kiraia walitangaza baadaye mchana kifo cha mtu wa tatu, mtu wa miaka 50 ambaye mwili wake ulikuwa karibu na mkondo huko Camarena, katika mkoa huo wa Toledo.

Utafutaji pia unaendelea ili kupata, katika eneo hilo, "mwanamke aliyetoweka kufuatia mafuriko (ya mto) huko Valmojado", pia kikosi cha walinzi wa raia kimebainisha.

Katika eneo jirani la Madrid, mwanamume mmoja pia amekuwa akitafutwa baada ya kusombwa usiku akiwa ndani ya gari lake na mto uliofurika katika mji wa Aldea del Fresno.

"Tunatafuta kwenye mto huu ili kujaribu kupata gari," msemaji wa idara ya huduma za dharura katika mkoa wa Madrid Javier Chivite amesema kwenye runinga ya umma.

Mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 10, ambaye alikuwa akisafiri naye, aliokolewa baada ya kupata hifadhi kwenye mti, mamlaka imesema. Mama yake na dada yake, ambao pia walikuwa kwenye gari, waliokolewa mapema.

"Maskini (mtoto) alikaa usiku kucha juu ya mti," amesema rais wa eneo hilo, Isabel Diaz Ayuso, akitembelea Aldea del Fresno, mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mvua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.