Pata taarifa kuu

Kundi la Hamas lawaachia huru mateka wawili

Mateka wawili waliokua wanashikiliwa na kundi la kigaidi la Hamas wanasemekana kuachiwa huru mapema leo na kukabidhiwa kwa jeshi la Israel.

Waombolezaji wakihudhuria mazishi ya Erik Kraunik, mkuu wa usalama wa Kibbutz Be'eri, kwenye makaburi ya Yehud, Israel ya kati.
Waombolezaji wakihudhuria mazishi ya Erik Kraunik, mkuu wa usalama wa Kibbutz Be'eri, kwenye makaburi ya Yehud, Israel ya kati. AP - Petros Giannakouris
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la wanamgambo limesema kuwa limewaachia huru wafungwa wawili wanawake , Nurit Cooper, mwenye umri wa miaka 79 na Yocheved Lifshitz wa umri wa miaka 85 na tayari wamekabidhibiwa kwa jeshi la Israel na wamepelekwa katika kituo cha afya.

Tangu mwanzoni mwa mzozo Israel imekua ikitoa wito wa kuachiliwa huru bila masharti mateka wote wanaoshikiliwa na kundi hilo.

Vilevile serikali ya Israel ilikuwa imewaambia watu  zaidi ya milioni moja kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini kabla ya uvamizi wa ardhini unaotarajiwa. Hii imesababisha mamia kwa maelfu ya watu kutafuta hifadhi katika eneo la  Khan Younis.

Haya yanajiri wakati huu Jeshi la Israel likifanya  uvamizi katika eneo la wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon, kujibu mashambulizi yake ya maroketi kaskazini mwa Israel.

Shambulio hilo lililenga miundombinu ya Hezbollah, ikiwa ni pamoja na mnara na jumba la kijeshi, kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya jeshi la Israel ya tovuti ya X, zamani ikiitwa Twitter.

Kwa miaka mingi, Israel imeimarisha kizuizi kati yake na eneo dogo la Wapalestina la Gaza.

Kundi la wapiganaji wa Hamas `ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wa Kipalestina ambayo yanadhibiti ukanda wa Gaza, eneo ambalo mara kwa mara hulitumia kukabiliana na Israel, taifa ambalo halilitambui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.